Habari Mpya

Mjumbe Maalamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Sudan kujitahidi kupata utulivu na amani mwaka huu wa 2010

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Sudan, Ashraf Qazi amewatolea wito watu wote wa Sudan kushikamana kutafuta amani zaidi 2010.

Eide ameonya kuendelea kwa mtafaruku wa kisiasa baada ya bunge la Afghanistan kulikataa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa

Kukataliwa na wabunge sehemu kubwa ya baraza hilo jipya la Rais Hamid Karzai ni pigo la kisiasa kwa nchi hiyo, amesema Mjumbe Maalumu wa KM nchini Afghanistan Kai Eide .