Habari Mpya

Mkuu mpya wa afisi ya UNAMID awasili Darfur

Mkuu mpya wa afisi ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMIND, Profesa Ibrahim Gambari aliwasili mjini El Fasher, Darfur Jumatatu, na kukutana na maafisa wa makao makuu na kukagua gwaride la walinda amani katika jimbo hilo.

Mkutano wa Kimataifa juu ya Haiti unafanyika Montreal

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka sehemu mbali mbali za dunia, akiwemo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hilary Clinton, wanakutana Montreal, Canada Jumatatu asubuhi, kwa mkutano wa kimataifa juu ya namna ya kusaidia kukarabati taifa la Haiti lililoharibiwa na tetemeko la ardhi.

UNCTAD: Uwekezaji wa Kigeni washuka sana mwaka 2009

Ripoti mpya ya Idara ya Biashara na maendeleo ya UM UNCTAD imegundua kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni FDI mwaka jana ulipungua katika kanda zote za dunia. Inaeleza kwamba mataifa yaliyoendelea yalishuhudia kuporomoka zaidi kwa uwekezaji mwaka 2008 na kuendelea kupunguka kwa mwaka 2009 kwa asili mia 41 zaidi.

Mswada una tishia kupunguza juhudi za kupambana na HIV Uganda

Mtaalamu maalumu wa UM kwa ajili ya masuala ya afya Anand Grover alionya Ijumaa kwamba mswada dhidi ya watu wa jinsia moja wanaopendana unaoanza kujadiliwa kwenye bunge la Uganda haukiuki tu haki msingi za binadamu za Uganda, bali utahujumu juhudi za kufikia lengo la kila mtu kupata huduma za kujikinga na HIV, matibabu na kusaidiwa.

Mashirika ya UM yanaendelea kutoa msaada Haiti

Shirika la afya Duniani WHO inasema kuna haja kubwa na muhimu wa kupatikana manasi wanaohitajika kusaidia katika huduma za afya kwa wathiriwa wa tetemeko la ardhi.

OCHA inasema hali ya usalama Haiti ni tulivu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura OCHA inasema hali katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince imebaki kua tulivu, ingawa kumekuwepo na matukio ya wizi wa ngawira na ghasia katika baadhi ya maeneo.

UNICEF yasema watoto wako hatarini kusafirishwa nje ya Haiti kinyume cha sheria

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto UNICEF limeonya kwamba watoto walonusurika kutokana na tetemeko la ardhi huko Haiti wako hatarini kuchukuliwa kinyume cha sheria na watu wapotofu.

Madaktari wanahofu idadi ya vifo kuongeza Haiti

Wafanyakazi wa huduma za dharura wanaonya kwamba idadi ya vifo huwenda ikaongezeka kutokana na watu walojeruhiwa vibaya sana na kutopata matibabu yanayohitajika.

KM asifu imani ya wanachi wa Haiti

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon alisifu imani na ustahmilivu wa wananchi wa Haiti kufuatia tetemeko lililosababisha maafa makubwa wiki iliyopita, akisema ana amini kwamba, kwa msaada wa jumuia ya kimataifa wataweza kukabiliana na maafa hayo.

UM unataraji uchumi dunia kufufua kidogo

Katika ripoti yake kuhusiana na hali ya uchumi duniani na matarajiyo yake UM umeeleza kwamba kuanzia robo ya pili ya mwaka jana, hali ya uchumi duniani imekua ikianza kurudi kua ya kawaida.