Habari Mpya

Wahamiaji wa JKK wakithiri katika taifa jirani kutafuta hifadhi baada kuzuka mapigano ya kikabila

Shirika la UM Juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti idadi ya raia wanaohajiri kutoka jimbo la Equateur, la kaskazini-magharibi katika JKK, inaendelea kuzidi kwa sababu ya kufumka kwa mapigano ya kikabila kwenye eneo lao.

EMG yatangaza rasmi sera ya kupunguza utoaji wa gesi chafu wa taasisi za UM

Vile vile kutoka Copenhagen, UM umetangaza rasmi utaratibu wa kupunguza gesi chafu zinazozalishwa na mashirika na taasisi mbalimbali za UM.

Kuwasili kwa KM Copenhagen kunatazamiwa kuhamasisha mataifa kukamilisha mapatano ya COP15

Ilivyokuwa majadiliano ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanaonekana kupwelewa, na yamezorota kwenye mabishano ya kiutaratibu, pamoja na mivutano na mgawanyo mkubwa wa kimasilahi baina ya nchi tajiri na mataifa maskini,

Hapa na pale

Ofisi ya UM Juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), imetangaza ripoti yenye kuelezea utaratibu wa sheria unaotumiwa na utawala wa kimabavu wa Israel katika kugawanya ardhi za WaFalastina ziliopo kwenye kanda mbalimbali za sehemu ya Ukingo wa Magharibi ya Mto Jordan, sehemu inayotambuliwa kama Eneo la C. Chini ya mfumo huo, WaFalastina huwa hawaruhusiwi kuendeleza ujenzi wa aina yoyote kwenye asilimia 70 ya maeneo yao. Wakati huo huo, ile asilimia 30 iliosalia ya maeneo ya WaFalastina, kumewekwa msururu wa vizuizi na vikwazo aina kwa aina ambavyo vinafuta, takriban, fursa zote za mtu kupata kibali cha kujenga. Kutokana na vikwazo kama hivi, makumi elfu ya WaFalastina wenye azma ya kujenga kwenye Eneo la C hunyimwa, kwa makusudi na kwa mipangilio, fursa ya kisheria ya kujenga na kutosheleza mahitaji ya makazi yao. Kwa sababu hizo,WaFalastina hulazimika kuendeleza ujenzi wa makazi yao bila ya kibali kutoka kwa watawala walowezi. Kwa hivyo, raia wa KiFalastina hukabiliwa na hatari ya majumba yao kubomolewa na, halafu, hung\'olewa makazi na watawala wa Israel waliokalia kimabavu ardhi yao.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ametangaza kwenye mkutano na waandishi habari Ijumatatu kwamba Wangari Maathai, mzalendo wa Kenya, aliotunukiwa Tunzo ya Amani ya Nobel na mtetezi wa mapinduzi ya kijani ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Amani wa UM mpya, atakayeshughulikia majukumu ya kuhifadhi mazingira na udhibiti bora wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani. KM aliwaambia wanahabari wa Makao Makuu, Profesa Maathai atatambulishwa rasmi kama Mjumbe wa Amani Ijumanne alasiri, kwenye taadhima maalumu itakaofanyika Copenhagen, ambapo Mkutano wa UM kuzingatia itifaki mpya ya kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa bado unaendelea na majadiliano yake. KM alisema uteuzi wa Profesa Maathai ulikuwa ni wa bora kabisa, kwa sababu ya mafanikio kadha aliopata kwenye bidii za muda mrefu za kutunza mazingira, na katika kuimarisha maendeleo. Profesa Wangari Maathai ni mwanamke wa KiAfrika pekee aliyetunukiwa Tunzo ya Nobel, na ameshatumikia Serikali ya Kenya kama waziri, na vile vile aliwahi kuwa mbunge, ni mwanataaluma na mtetezi shupavu wa haki za wanawake kwa zaidi ya miaka arobaini.

Wataalamu wakusanyishwa Geneva na UNCTAD kuzingatia ushirikiano wa mataifa ya Kusini kuhudumia maendeleo

Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) linalosimamia ukuzaji wa biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea, ili kupiga vita ufukara na hali duni, limeanzisha mjini Geneva mkutano wa siku tatu, wenye makusudio ya kutafuta taratibu zinazofaa kuimarisha ushirikiano

Mjumbe wa UM apongeza usajili wa amani wa wapiga kura Sudan

Mjumbe Mkuu wa UM kwa Sudan, Ashraf Jehangir Qazi, ametangaza kukaribisha mwisho mzuri, wa utaratibu wa kusajili wapiga kura, kwa uchaguzi wa vyama vyingi, utakaofanyika nchini Sudan mwaka ujao. Asilimia 75 ya watu waliofikia umri wa kupiga kura walirajisiwa, sawa na raia wa Sudan milioni kumi na tano. Baina ya tarehe 1 Novemba mpaka Disemba 07 (2009), mamilioni ya watu walifanikiwa

Baada ya mazungumzo kusimamishwa kwa muda Copenhagen, wajumbe wa kimataifa warudia tena majadiliano

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, au Mkutano wa COP 15, yalisimamishwa kwa muda baada ya nchi wanachama wa Kundi la G-77, linalowakilisha mataifa yanayoendelea, zilipoamua kutoshiriki kwenye mazungumzo, hususan nchi za KiAfrika. Wawakilishi wa bara la Afrika waliopo

UM yathibitisha robo tatu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na majanga ya kimaumbile

Margareta Walhstrom, Mjumbe Maalumu wa KM anayehudumia Mpango wa Kupunguza Athari za Maafa amenakiliwa akisema hali ya hewa mbaya kabisa iliojiri ulimwenguni, katika miezi 11 iliopita, ndio matukio yaliosababisha asilimia 75 ya vifo vinavyoambatana na majanga na maafa ya kimaumbile.

Wakati wa kukamilisha itifaki mpya kudhibiti athari za hali ya hewa ni sasa, anasema KM

Kwenye mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, Ijumatatu asubuhi, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu kwa viongozi wa dunia wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Copenhagen, unaowasihi waongeze, mara mbili zaidi, juhudi zao za