Habari Mpya

UNHCR imetangaza watu 74,000 wa Pembe ya Afrika wamehajiri Yemen 2009 kuomba hifadhi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti raia 74,000 waliwasili kwenye mwambao wa taifa la Yemen mwaka huu, kutoka eneo la Pembe ya Afrika, watu waliokuwa wakikimbia hali ya mtafaruku uliozuka na kujiepusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na uegugeu wa kisiasa, hali duni ya maisha, ikichanganyika vile vile na baa la njaa na ukame.

Mtetezi wa Haki za Binadamu Sahara Magharibi aruhusiwa kurejea nchini

Taarifa iliotolewa na KM Ban Ki-moon, baada ya saa sita za usiku ya Ijumaa, imeeleza kuwa amefarajika na pia kupata nafuu baada ya kupokea ripoti ilioleza mtetezi wa uhuru wa taifa la Sahara ya Magharibi, Aminatou Haidar, aliruhusiwa kurejea kwao kwenye mji mkuu wa Laayoun.

Mashirika ya UM yajihusisha Kenya kudhibiti mripuko wa kipindupindu Turkana Mashariki

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti Alkhamisi jioni kwamba taasisi kadha za UM zinazohudumia misaada ya kiutu, hivi sasa zinajitahidi kuipatia Serikali ya Kenya misaada ya dharura inayohitajika kupambana na mripuko wa maradhi ya kipindupindu, yaliozuka kwenye eneo la kaskazini-magharibi, ambapo tumearifiwa watu karibu 30 walifariki kutokana na ugonjwa huo, kwenye zile sehemu za mbali zenye matatizo kuzifikia.

Viongozi wa Dunia wamo mbioni kuleta maafikiano ya kuridhisha kutoka Mkutano wa COP15

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa UM wa kuleta mapatano yatakayosaidia Mataifa Wanachama kudhibiti bora, kipamoja, athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu, Ijumaa yalishindwa kuwasilisha maafikiano ya kuridhisha, yaliotarajiwa kutiwa sahihi na viongozi wa Kitaifa na serikali 120 ziada waliokusanyika sasa hivi kwenye mji wa Copenhagen, Denmark.

Shughuli za Baraza la Usalama kwa Alkhamisi

Mapema asubuhi ya leo, Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa shughuli za Ofisi ya UM juu ya Mchanganisho wa Huduma za Amani Burundi (BINUB) ambazo zinatazamiwa kuendelezwa hadi mwisho wa mwaka 2010.

Ripoti ya Kamisheni ya Uchunguzi wa vurugu la Septemba katika Guinea imekabidhiwa rasmi KM

KM amekabidhiwa ripoti ya Kamisheni Maalumu ya Uchunguzi ya Kimataifa kuhusu vyanzo vya matukio ya fujo mnamo tarehe 28 Septemba 2009 katika taifa la Afrika Magharibi la Guinea, ambapo raia wapinzani kadha waliripotiwa kuuawa kihorera na vikosi vya ulinzi, kufuatia maandamano yaliofanyika kwenye mji mkuu wa Conakry.

KM akutana na viongozi wanaohudhuria COP15

KM Ban Ki-moon leo alianzisha mazungumzo ya kina, ya pande mbili, na viongozi kadha wa kadha wa kimataifa, ikijumlisha Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jinbao. Alipokutana na waandishi habari Alkhamisi,

Mkutano wa Mabadiliko ya Halihewa unanyemelea hatima

Wakati huo huo, majadiliano yameanzishwa tena kuhusu maafikiano mapya ya kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa, baada ya mzoroto na mivutano ya siku mbili baina ya mataifa yenye maendeleo ya viwanda na mataifa yanayoendelea.

Matumaini yafifia juu ya itifaki ziada kutoka Mkutano wa COP15

Taarifa tulizopokea kutoka Mkutano wa COP15, zinasema matumaini ya kuwakilisha itifaki ziada, kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, yanaanza kufifia,

Hapa na pale

Alkhamisi asubuhi, mataifa 11 yaliripotiwa kuidhinisha na kuridhia Mapatano ya Kimataifa ya 2006 juu ya Mbao za Tropiki (2006 International Tropical Timber Agreement). Nyaraka za Mapatano ziliokusudiwa kukabidhiwa KM, ziliwakilishwa kwenye tafrija iliofanyika katika Ofisi ya UM juu ya Masuala ya Sheria. Mataifa 11 yalioridhia Mapatano ya Mbao za Tropiki ni kama ifuatavyo: Bulgaria; Jamhuri ya Ucheki; Finland; Ujerumani, Ireland; Ureno; Romania; Slovakia; Slovenia na Uspeni. Mapatano ya Mbao za Tropiki, bado hayajakuwa chombo rasmi cha kimataifa na sasa hivi kinajumlisha Makundi Yalioridhia mapatano kutoka nchi arobaini na moja.