Habari Mpya

Mashambulio ya majengo ya UM Ghaza lazima yachunguzwe na tume huru, UNRWA yasisitiza

Kadhalika Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), limesema linataka kufanyike uchunguzi halali, ulio huru, kuhusu mashambulio ya majengo ya UNRWA yaliotoa hifadhi kwa watu waliokimbia mapigano, katika Jabaliya, ambapo watu 40 ziada waliuawa wiki hii.

ICRC yashtumu Israel kwa kukiuka kanuni za kimataifa kuhusu majeruhi wa mapigano.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imeripoti leo, kwa kupitia msemaji wake Geneva, Dominik Stillhart, kwamba majeshi ya Israel “yameshindwa kutekeleza majukumu yao, chini ya sheria za kiutu za kimataifa za kuhudumia majeruhi wa vita.”

WHO inasema huduma za afya Ghaza zimevurugika

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti huduma za afya ya jamii katika Tarafa ya Ghaza zinahitajia, kidharura vifaa, madawa na wafanyakazi.

Huduma za kugawa chakula Ghaza zimesimamishwa, kwa muida, na UM

KM ameshtumu mashambulio ya vikosi vya Israel dhidi ya misafara ya malori ya UM, yaliokuwa yamechukua misaada ya kiutu kwa wakazi wa eneo la Ghaza, ambapo wafanyakazi wawili wa UNRWA waliuawa, licha ya kuwa wenye madaraka wamepatiwa taarifa kamili kuhusu misafara hiyo.

UNHCR yaihadharisha BU juu ya matatizo ya kuhifadhi wahamiaji duniani

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) asubuhi ya leo amehutubia Baraza la Usalama kuhusu vizingiti vinavyokabili shirika katika kuhudumia makumi milioni ya wahamiaji waliong’olewa makwao katika sehemu mbalimbali za dunia, kutokana na hali ya mkorogano na hatari iliopamba sasa hivi kwenye mazingira ya kimaaifa.

Wahamiaji wa ndani milioni 9.1 wanaishi sasa Afrika ya Kati na Afrika Mashariki, inasema UM

Ripoti mpya ya UM, iliotolewa mapema wiki hii, kuhusu wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) waliopo katika maeneo ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati, imethibitisha kwamba kumalizikia mwezi Disemba 2008, jumla ya wahamiaji hao ilikuwa milioni 9.1.

WFP yasihi mapigano yasitishwe ili itathminie mahitaji ya umma wa Ghaza

Hii leo, Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa mwito maalumu, kwa makundi yanayohasimiana katika eneo la Tarafa ya Ghaza, kusitisha mapigano na kuruhusu wahudumia misaada ya kiutu angalau kupata “upenu wa kupumua” utakaowawezesha kutathminia vyema mahitaji halisi ya umma waathirika katika Ghaza, ili baadaye kuwapatia wakazi hawo misaada ya kihali, ya kunusuru maisha.

Taasisi za Umoja wa Mataifa zinakutana kusailia mzozo wa Ghaza

Baraza la Usalama limekutana leo hii, kwa mara ya pili tena, kuanzia saa tano ili kuendelea na majadiliano ya hadhara juu ya mzozo wa kiutu uliolivaa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.

Makundi yanayofarakana katika JKK yahimizwa kukomesha haraka uhasama wao

Duru ya Tatu ya Mazungumzo ya Nairobi juu ya usuluhishi wa mfarakano baina ya Serikali na kundi la Congrès National pour la Défense du People (CNDP) kuhusu eneo la mashariki katika JKK, imeanza majadiliano muhimu hii leo yalioongozwa na Mpatanishi Mwenzi, Raisi mstaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania kwa sababu Mjumbe Maalumu wa KM kwa Eneo la Maziwa Makuu, Olusegun Obasanjo, hakuweza kuhudhuria. Mkapa aliwaambia wajumbe

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe anaomba mazungumzo ya upatanishi yafufuliwe

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, Ijumatano ametoa mwito kwa Raisi wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe unaomtaka atayarishe mazungumzo ya faragha, ya upatanishi, baina ya wajumbe wa upinzani na Raisi Robert Mugabe, ili kufufua tena zile juhudi za kusuluhisha maafikiano ya kugawana madaraka, yaliotiwa sahihi mwezi Septemba 2008.~