Habari Mpya

Baraza la Haki za Binadamu laandaa tume ya kuchunguza ukiukaji wa haki katika Ghaza

Raisi wa Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu, naye anajiandaa pia kutayarisha mazungumzo ya dharura ya kuteua wajumbe wa tume maalumu ya uchunguzi, itakayopelekwa Ghaza kuthibitisha yale madai ya kwamba majeshi ya Israel yamekiuka haki za binadamu kutokana na opereshenzi zao kwenye eneo husika.

Ofisa wa UNRWA anasema hali Ghaza ni ya kutisha mno

John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina kwenye Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameiambia Ofisi ya UM, Geneva, hii leo, kwa kutumia njia yasimu, ya kwamba mipangilio ya kuhudumia misaada ya kihali Ghaza, kwa umma muhitaji, imevurugwa kwa sasa, kwa sababu ya kuendelea kwa mapigano, hali ambayo vile vile alisema imeongeza khofu na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Ghaza pamoja na umma wa eneo jirani.

Watoto wa Ghaza lazima walindwe, Kamati ya Haki ya Mtoto yasihi

Kamati ya UM juu ya Haki ya Mtoto, yenye wajumbe 18, ambayo inakutana sasa Geneva, imetoa ripoti yenye kubainisha wasiwasi mkubwa juu athari haribifu, kiakili, dhidi ya watoto wadogo, kutokana na vurugu la mapigano liliopamba kwenye eneo la Tarafa ya Ghaza.

Hapa na Pale

KM Ban Ki-moon Ijumanne asubuhi alikuwa na mazungumzo ya ushauri, ya faragha, na wawakilishi wa Mataifa Wanachama 15 wa Baraza la Usalama kuhusu safari yake ya Mashariki ya Kati, yenye madhumuni ya kuhamasisha makundi husika na uhasama uliozuka kwenye Tarafa ya Ghaza, kusimamisha mapigano haraka, kama ilivyopendekezwa na azimio nambari 1860 (2009), na baadaye kuyawezesha mashirika yenye kuhudumia misaada ya kiutu kukidhia mahitaji ya umma waathirika na mapigano.

LRA inaendelea kutesa wasio hatia katika JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kukhofia usalama, na hali, kijumla, kutokana na mashambulio ya karibuni ya kundi la waasi wa Uganda la LRA kwenye Jimbo la Orientale, katika JKK.

Haki za binadamu zakiukwa Ghaza, inasema UM

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu baada ya majadiliano ya siku mbili, kwenye kikao cha dharura, Ijumatatu mjini Geneva limepitisha azimio lenye kulaani vikali operesheni za kijeshi zinazoendelea sasa hivi za vikosi vya Israel kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Ghaza.

WFP kuanzisha operesheni za kuokoa maisha ya mamia elfu Ghaza

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha huduma ijulikanayo kama Operesheni za Kamba ya Kuokolea Ghaza, yenye lengo la kuhudumia watu wenye njaa ambao idadi yao inaendelea kuongezeka kila kukicha, tangu Israel kuanzisha mashambulio yake karibu wiki tatu zilizopita.

ICC imeanza kusikiliza mashtaka dhidi ya JP Bemba

Kuhusu habari nyengine, Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo imeanzisha kusikiliza mashtaka dhidi ya Jeane-Pierre Bemba, raia wa JKK, aliyetuhumiwa kushiriki kwenye makosa ya vita na jinai dhidi ya utu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK) kuanzia 25 Oktoba, 2002 hadi 15 Machi, 2005. Anatuhumiwa kuongoza jeshi la mgambo la MLC liliofanyisha

Kamati ya Haki ya Mtoto yakutana Geneva

Kamati juu ya Haki ya Mtoto imeanzisha kikao cha 50 mjini Geneva leo Ijumatatu kuzingatia ripoti kuhusu utekelezaji wa haki hizo katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea ya Kaskazini), JKK, Malawi, Uholanzi, Chad na vile vile Moldova

Hapa na Pale

Kwenye mkutano wa, awali, wa mwaka na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, KM Ban Ki-moon aliwasilisha ujumbe maalumu kuhusu vurugu liliopamba eneo la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, ujumbe ambao alisema ulio na lugha isio ngumu, ulio wazi na wa maana, wenye kuyanasihi makundi yenye kuhasimiana “kukomesha mapigano, haraka .. sasa hivi”. Alikumbusha kwamba watu wingi wameshafariki kutokana na uhasama huo katika Ghaza, hali ambayo imewafanya raia wa Israel na umma wa WaFalastina kujikuta wanaishi “maisha ya khofu” kila kukicha. Alisema mazingira ya Tarafa ya Ghaza, ndipo penye chimbuko na “msingi wa umma wa KiFalastina unaoshuhudia maangamizi: nyumba