Habari Mpya

Hapa na Pale

Kwenye mkutano wa hadhara, asubuhi, na watumishi wa UM, KM Ban Ki-moon alisema mgogoro uliopamba sasa hivi katika Tarafa ya Ghaza, na pia Israel kusini, umesasbabisha uharibifu zaidi katika saa 48 zilizopita. Alisema mateso na maumivu yaliowakumba raia yanashtusha, na alisisitiza operesheni za vikosi vya Israel zilizoanzishwa Ijumamosi ndani ya Ghaza yenyewe, zimeharibu kabisa hali katika eneo hilo.~

BU na KM wasailia hali baada ya kuingia Ghaza kwa majeshi ya Israel

KM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa na msemaji wake, alinakiliwa akisema ameingiwa na “wasiwasi mkubbwa kuhusu athari mbaya kufuatia kuanzishwa kwa operesheni za ardhini za vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza” Ijumamosi (03/01/2009), wakati ambao Baraza la Usalama (BU) vile vile liliamua kuitisha kikao cha dharura kuzingatia hali hiyo ya uhasama Ghaza.

Kumbukumbu za majadiliano kuzingatia muongezeko wa vurugu katika Ghaza

Ifuatayo ni kumbukumbu ya kikao cha Baraza la Usalama, kilichofanyika Ijumatano kwenye Makao Makuu ya UM, kuanzia saa 12:40 magharibi hadi saa 2:45 usiku.~

Wataalamu wa haki za binadamu watoa mwito wa kuhifadhi raia Ghaza

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uratibu ya Wakariri Huru wa Haki za Binadamu, Bibi Asma Jahangir, leo amewasilisha taarifa inayosema wataalamu wanachama wa Kamati “wameshtushwa kwa kina juu ya kuendelea kwa wimbi la vurugu kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.”

UNRWA yaomba dola milioni 34 kuhudumia misaada ya kiutu katika Ghaza

Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limetoa ombi kwa wahisani wa kimataifa la kufadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 34, ili kukidhi, halan, mahitaji ya umma wa Tarafa ya Ghaza, mahitaji ambayo yanaendelea kukithiri tangu mashambulizi kuanzishwa na vikosi vya Israel kwenye eneo mnamo tarehe 27 Disemba 2008.~~

Ofisa wa UNRWA anasema raia wa Ghaza washindwa kupokea misaada ya kihali kwa sababu ya mashambulio ya Israel

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Samir Imtair AlDarabi leo asubuhi alimwuliza Sami Mshasha, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la UNRWA kama wamefanikiwa kugawa chakula, kwa umma muhitaji wa Ghaza, katika siku za karibuni:~

Mjumbe wa KM Usomali alaani vikali mauaji ya kihorera ya watu mashuhuri nchini

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould Abdallah kwenye taarifa iliotolewa leo Ijumaa, amelaani mauaji ya karibuni ya watu mashuhuri watatu katika Usomali, na kusisitiza kwamba vitendo vya “uhalifu” na jinai isiyokhofu kuadhibiwa wala kuumia, ni lazima vikomeshwe haraka nchini humo.

MONUC yakataa hadharani madai ya Nkunda

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kukanya madai ya Laurent Nkunda, kiongozi wa kundi la waasi wa CNDP aliyoyabainisha kwenye barua aliomtumia Mjumbe Maalumu wa KM, Alan Doss, madai yaliyosema kwamba vikosi vya Serikali vimeonekana kuongezwa kwenye ile sehemu ya mapigano, katika eneo la mashariki la Kibati, liliopo kilomita 10 kaskazini ya mji wa Goma.

SALAMU ZA MWAKA MPYA

WASIKILIZAJI, ALKHAMISI YA LEO, TAREHE MOSI JANUARI 2009, OFISI ZOTE ZA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NEW YORK ZIMEFUNGWA, KUADHIMISHA SIKU KUU YA MWAKA MPYA.~