Habari Mpya

UNICEF inasema watoto wanavia kwa sababu ya upungufu sugu wa chakula

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) nayo pia imewasilisha ripoti maalumu inaozingatia athari za ukosefu wa chakula kwa watoto wachanga.

Mchanganyiko wa vitega uchumi na nia ya kisiasa huweza kufyeka njaa - FAO

Ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), iliochapishwa rasmi leo hii, yenye kutathminia maendeleo yaliofanyika kwenye nchi kadha inazozishughulikia, imebainisha kwamba idadi ya watu wasiopata chakula cha kutosha iliteremka kwa kiwango kikubwa, na cha kutia moyo.

UM umeteua Julai 18 kuwa ni Siku Kuu ya Kimataifa Kumhishimu Nelson Mandela

Ijumanne, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kusailia mada muhimu inayohusu "utamaduni wa amani", Mataifa Wanachama yalipitisha, bila kupingwa, azimio la kuadhimisha tarehe 18 Julai, kila mwaka, kuwa ni ‘Siku ya Kimataifa Kumhishimu Nelson Mandela\'.

Hapa na Pale

KM Ban Ki-moon siku ya leo anazuru Washington D.C. ambapo asubuhi alikutana na maofisa wa Makao Makuu ya Raisi wa Marekani (White House) wanaohusika na masuala ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni. Alasiri KM vile vile alikutana na viongozi wa Bunge la Marekani na walishauriana juu ya mada zinazofungamana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Raia waliong'olewa makazi JKK wafarajiwa kihali na UM

Taarifa mpya zimefichuka karibuni, kuhusu mapigano ya kikabila yaliofumka mwezi Novemba, kwenye jimbo la Equateur, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

Lengo la MDGs kupambana na UKIMWI linafanyiwa mapitio na UNAIDS

Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS), kwenye makala iliochapishwa wiki hii katika Jarida juu ya UKIMWI, imezingatia kwa makini zaidi, suala la kama jamii ya kimataifa itafanikiwa kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika 2015, kwa kulingana na pendekezo rakamu ya sita ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

WHO itafadhaliwa dozi milioni 50 za chanjo kudhibiti A/H1N1 kwa nchi maskini

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hii leo kwamba kampuni ya GlaxoSmithKline, inayohusika na huduma ya matunzo ya afya, imetiana sahihi na UM, mapatano rasmi ya kufadhilia dozi milioni 50 za dawa ya kupambana na homa ya mafua ya A/H1N1 kimataifa.

OCHA inasihi, misaada ya dharura yahitajika kuunusuru umma wa Usomali na majanga ya kiutu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeihimiza jumuiya ya kimataifa, kuharakisha michango ya dharura inayotakikana kunusuru maisha kwa raia wa Usomali.

Nchi maskini 31 zimedhurika na bei ya juu ya chakula: FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwamba ulimwengu unakabiliwa na uhaba mkubwa, na wa hatari wa chakula, ulioathiri vibaya sana nchi 31.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amesema ana matumaini serikali wanachama katika UM zitaweza kufikia mapatano juu ya masuala ya kimsingi, kwenye mkusanyiko wa Mkutano wa Copenhagen." Janos Pasztor, Mkurugenzi wa Tume ya KM Kushughulikia Masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa amenakiliwa akisema ana imani mapatano anayoyazungumzia KM yatawakilisha "maudhui yenye sheria ya kuongoza utendaji wa kimataifa unaotakikana kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia."