Habari Mpya

Hapa na pale

Ripoti mpya ya Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo imeripoti ya kuwa idadi ya watafiti na wachunguzi wa kitaaluma katika mataifa yanayoendelea imeongezeka, kwa kiwango cha kutia moyo katika miaka ya karibuni. Ripoti ilieleza baina ya miaka ya 2002 hadi 2007, idadi ya watafiti katika nchi zinazoendelea ilizidi kwa asilimia 56, ikimaanisha nchi nyingi zenye uchumi haba zimetambua umuhimu wa kuendeleza tafiti zinazowasilisha ubunifu unaoleta mageuzi ya kiteknolojia kwenye maendeleo yao.

Viwango vya gesi chafuzi duniani vinaripotiwa kufurutu ada

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwenye ripoti yake mpya iliochapisha Ijumatatu, imeeleza kwamba kiwango cha ile hewa chafu inayotupwa kwenye anga, kinaeendelea kukithiri katika dunia.

UM imethibitisha mabaki ya mtumishi wa UM aliyepotea miaka mingi Lebanon

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon amearifiwa kupatikana kwa mabaki ya Alec Collett katika Lebanon mashariki.

Mtetezi wa haki za watoto asema kasumbuliwa sana na ripoti za watoto wanaoshirikishwa na wapambanaji katika Sudan

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano, ameripotiwa kuwa ana wasiwasi juu ya taarifa alizopokea, zinazoonyesha watoto walio chini ya umri wa utu uzima, wameruhusiwa kujiunga na makundi ya waasi wa katika Sudan.

Urajisi wa wapiganaji wa zamani waanzishwa rasmi katika Darfur

Vile vile kuhusu Sudan, mnamo siku ya leo, katika mji wa El fasher, wapiganaji wa zamani 5000 kutoka makundi kadha yaliotia sahihi Mapatano ya Amani kwa Darfur, wameanza urajisi wa kujumuishwa kwenye maisha ya kawaida nchini.

Fafanuzi fupi juu ya mkutano wa UNIFEM kwa wanawake wa Darfur Kaskazini

Mnamo wiki iliopita, wanawake 500 ziada, kutoka fani na kazi mbalimbali walikusanyika katika Chuo Kikuu cha El Fasher, Darfur Kaskazini kusailia amani na utulivu kwenye eneo lao, na taifa, kwa ujumla.

Mazungumzo ya Redio ya UM na mshindi wa mashindano ya picha ya UNDP/Olympus/AFP kutoka Kenya

Ijumatano raia wawili wa kutoka Kenya, pamoja na mzalendo mwanamke kutoka Morocco, walitunukiwa zawadi maalumu, kwa picha zao zilizoonyesha namna watu wa kawaida barani Afrika, wanavyoshiriki kwenye harakati za kutunza na kuhifadhi mazingira - ikijumlisha zile shughuli za kupandisha miti, na huduma za kuigeuza mifuko ya plastiki, iliotupwa kwenye majaa baada ya kutumiwa, kuwa mikoba ya pochi na vikapu, ikiwa miongoni mwa kadhia muhimu zinazochangia kimataifa katika kupunguza athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkataba wa Haki za Mtoto wakamilisha miaka ishirini

Tarehe ya leo, Novemba 20, 2009 inawakilisha kumbukumbu ya maiaka 20 ya Mkataba juu ya Haki za Mtoto.

Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2009 - UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limewasilisha ripoti muhimu Alkhamisi inayosailia: Hali ya Watoto Duniani.

Ripoti ya IFRC inasihi, huduma za misaada ya kihali Afrika zahitajia marekibisho ya hali ya juu

Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC), iliochapishwa hii leo, imeonya kwamba misaada ya kiutu inayofadhiliwa bara la Afrika ni ya gharama kubwa, na mara nyingi inashindwa kukidhia mahitaji yanayoendelea kupanuka, kwa zile jamii dhaifu kihali, ziliopo katika sehemu mbalimbali za Afrika.