Habari Mpya

Uganda: Mratibu Mkuu wa UM juu ya Misaada ya Kiutu asihi umuhimu wa kinga ya mapema dhidi ya hatari ya maafa

John Holmes, Naibu KM juu ya Misaada ya Kiutu na Masuala ya Kufarajia Misaada ya Dharura, alipozuru jimbo la Karamoja, Uganda kaskazini Ijumaa ya leo, alisihi juu ya umuhimu wa kupunguza hatari ya maafa kwa kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye sehemu hizo za nchi.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ayapongeza Mataifa ya Afrika kwa kuidhinisha chombo kipya cha sheria kulinda haki za wahamiaji wa ndani

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amekaribisha, kwa furaha kuu, maafikiano ya kuwa na mkataba wa kihistoria kuhusu hifadhi ya wahamiaji wa ndani ya nchi katika Afrika, ambao uliidhinishwa leo hii kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Wakuu wa Mataifa Wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Uganda.

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limechapisha taarifa inayojulikana kama "taarifa ya utaratibu wa sanduku la vifaa" juu ya haki ya kupata chakula, mfumo ambao umekusudiwa kuzipatia nchi wanachama, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na wadau wengineo hati zinazofaa kutumiwa kutetea haki ya kupata chakula, haki ambayo ni sawa na haki za kimsingi za wanadamu.

UM kuhadharisha, watu milioni sita ziada Ethiopia wanahitajia misaada ya chakula kuwavua na janga la njaa

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti Ethiopia imezongwa na mshtuko mkuu wa maafa yenye kuathiri hali ya chakula kwa watu milioni 6 nchini.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya NEPAD azungumzia mwelekeo unaohitajika kusukuma mbele maendeleo Afrika

Mapema wiki hii, kabla ya kuzungumzia kikao cha Baraza Kuu la UM, kusailia ripoti kadha za KM, na kutoka wajumbe wa kimataifa na mashirika ya UM zilizozingatia huduma za kukuza maendeleo katika Afrika, Dktr Ibrahim Assane Mayaki, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo kwa Afrika (NEPAD), alifanya mahojiano maalumu na waandishi habari waliopo Makao Makuu.

Homa ya nguruwe wa Afrika imeripotiwa kutapakaa Urusi Kaskazini, imehadharisha FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza ya kuwa ule ugonjwa maututi wa nguruwe, wenye kutambulika kama homa ya nguruwe wa Afrika (ASF), mnamo tarehe 20 Oktoba umegunduliwa katika eneo la St Petresburg, liliopo kaskazini-magharibi katika Urusi, kilomita 2,000 kutoka kusini ya Urusi ambapo maradhi haya yalikutikana hapo kabla.

Waathirika milioni sita ziada wa ukame Ethiopia wanahitajia misaada ya dharura ya chakula

Serikali ya Ethiopia na mashirika ya kimataifa yenye kuhusika na misaada ya kiutu yametangaza kunahitajika mchango wa dharura ziada wa dola miilioni 175 kwa mwaka huu, kuhudumia kihali watu milioni 6.2 walioathirika sana na mavuno haba na ukame wa muda mrefu uliosakama katika Ethiopia katika kipindi cha karibuni.

Walinzi amani wa UNAMID wasaidia kukomesha mapambano ya kikabila Darfur Kaskazini

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti walinzi amani wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) walilazimika wiki hii kuingilia kati kuzuia mapambano makali ya kikabila yaliotukia karibu na eneo la Shangil Tobaya, Darfur Kaskazini baina ya makabila ya Zaghawa na Birgid.

Makampuni ya bima yajiunga na UM kudhibiti 'uchumi wa kijani'

Kampuni za kimataifa za bima, zinazodhibiti rasilmali inayogharamiwa matrilioni ya dola, zimejiunga na wataalamu mashuhuri wa kimataifa kwenye uchunguzi, wenye kuungwa mkono na UM, wa kuhakikisha viwanda vinatumia utaratibu unaosarifika na usiochafua mazingira.

IFAD inasema uhamishaji wa fedha wa wafanyakazi wa Afrika waliopo nje unaweza kustawisha maisha ya vijiji

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) limewasilisha ripoti mpya inayozingatia athari za kiuchumi zinazofungamana na uhamishaji wa malipo ya fedha, unaoendelezwa na wafanyakazi wa kutoka Afrika waliopo nchi za kigeni.