Habari Mpya

Idadi ya vifo kupanda kwa wahamiaji Waafrika waliojaribu kuvuka Ghuba ya Aden

Mnamo saa 48 zilizopita imeripotiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwamba watu 16 walifariki na 49 wengine wamepotea, na kudhaniwa ni maututi kwa sababu ya matukio matatu tofauti yanayoambatana na mashua zilizokuwa zikivusha watu kimagendo kwenye Ghuba ya Aden wahamiaji waliojumlisha wale waliotoka Usomali na raia wengine wa kutoka Afrika.

Kutoruhusu wahamiaji waliokwama baharini kuingia nchini kwaharamisha sheria ya kimataifa, ameonya Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay kwenye hotuba aliotoa Ijumanne mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, aliwashtumu vikali wale wenye mamlaka pamoja na manahodha wa meli kadha wanaoharamisha sheria za kimataifa wanapowakatalia kuwachukua wale wahamiaji walioachwa kutangatanga baharini.

BK limepitisha azimio juu ya 'haki ya kulinda raia'

Baraza Kuu la UM limepitisha, kwa pamoja, lile Azimio la \'Wajibu wa Mataifa Kulinda Raia\' wakati wajumbe wa kimataifa walipokaribia kufunga kikao cha 63 katika Ijumatatu alasiri.

Tume ya UM yagundua makosa ya jinai yalitendeka na pande zote Ghaza

Asubuhi ya leo, Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini aliyeongoza Tume Maalumu ya Baraza la Haki za Binadamu iliodhaminiwa jukumu la kutathminia taathira za mashambulio ya vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza, aliwasilisha matokeo ya uchunguzi wao kwenye mkutano na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu.

Raisi wa BK anasema UM unahitajia marekibisho adhimu kikazi

Ijumatatu, wakati Baraza Kuu (BK) la UM lilipokamilisha kikao chake cha mwaka, cha 63, wajumbe wa kimataifa waliarifiwa kwenye hotuba yake ya kufunga kikao, ya Raisi wa Baraza, ya kuwa UM unahitajia kufanyiwa marekibisho ya dharura na mabadiliko ya jumla ili uweze kuendeleza shughuli zake kwa mafanikio.

Mabwawa ya maji ya Ghaza yahatarishwa kuporomoka

Mabwawa ya maji yaliopo chini ya ardhi, ambayo WaFalastina milioni 1.5 wanaoishi katika eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza hutegemea kwa kilimo na matumizi, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) mabwawa haya yanakaribia kuporomoka.

Angelina Jolie ashtushwa na hali ngumu kwenye kambi ya wahamiaji wa Usomali mipakani Kenya

Angelina Jolie, msanii maarufu wa michezo ya sinema na Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) alifanya ziara ya siku moja, mnamo mwisho wa wiki iliopita, katika kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo kwenye mpaka kati ya Kenya na Usomali.

Baraza la Haki za Binadamu laanzisha kikao cha kawaida Geneva

Baraza la Haki za Binadamu leo limeanza rasmi kikao chake cha kawaida cha kumi na mbili mjini Geneva. Mkutano ulianza kwa majadiliano ya hadhi ya juu ambapo wawakilishi wa Sri Lanka, Marekani na Thailand walihutubia.

Shughuli za "kufufua amani" Sierra Leone zaashiriwa kukabiliwa na vizingiti ziada kwa siku zijazo

Baraza la Usalama asubuhi lilikutana kuzingatia juu ya shughuli za Ofisi ya Muungano wa Huduma za Ujenzi Amani katika Sierra Leone (UNIPSIL).

Mkuu wa IAEA apendekeza taasisi yao ipatiwe madaraka zaidi kuendeleza shughuli zake

Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la IAEA, Mohamed ElBaradei kwenye risala alioitoa mbele ya kikao cha 53 cha Baraza Kuu la IAEA alizisihi nchi wanachama kuipatia taasisi yao "madaraka zaidi ili kuzuia kihakika, na kwa mafanikio, uenezaji wa silaha za kinyuklia katika ulimwengu" hususan kwenye usimamizi wa utekelezaji wa kanuni za Mkataba wa NPT.