Habari Mpya

Mkurugenzi wa taasisi ya ICGLR azungumza na Redio ya UM juu ya shughuli za shirika lao

Siku ya leo, Ijumatatu tarehe 21 Septemba, ofisi za UM za Makao Makuu zimefungwa rasmi kwa sababu ya Siku Kuu ya Eid al Fitr. Kwa hivyo, badala ya taarifa za habari za kila siku, leo tumekuandalieni kipindi maalumu kuhusu shughuli za Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGRL) yenye makao yake rasmi mjini Bujumbura, Burundi. Makala hii itaongozwa na mimi AWK.

Haki za wahamaji kwenye vizuizi vya idara za uhamiaji zinahitajia marekibisho, anasema Pillay

Alkhamisi mjini Geneva, Baraza la Haki za Binadamu, kwenye pambizo za kikao chake cha mwaka, iliandaa warsha maalumu kuzingatia kwa kina, masuala yanayohusu haki za wahamiaji na wahamaji wanaowekwa kwenye vituo vya kufungia watu vya idara za uhamiaji, haki ambazo katika miaka ya karibuni zilionekana kukiukwa kihorera na mataifa pokezi ya wahamaji.

Siku Kuu ya Amani Kimataifa

Tarehe 21 Septemba itaadhimishwa na UM kama ni Siku Kuu ya Amani Kimataifa. Ilivyokuwa Ijumatatu ofisi za UM zitafungwa hapa Makao Makuu kusherehekea Eid al Fitri, Siku Kuu ya Amani inahishimiwa leo Ijumaa, Septemba 18.

Kwenye mazungumzo na Mkuu wa UA, KM amerudia ahadi ya UM kuisaidia AMISOM Usomali

Ijumaa KM Ban Ki-moon alizungumza,kwa simu, na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (UA), Jean Ping kuhusu shambulio la kujitoa mhanga liliotukia Alkhamisi kwenye makao makuu ya vikosi vya amani vya AMISOM mjini Mogadishu.

Kamishna wa Haki za Binadamu ashtushwa na shambulio la kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani Yemen

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu Ijumaa ilioleza kusumbuliwa sana na taarifa za watu walioshuhudia shambulio la ndege za Yemen, liliotukia tarehe 16 Septemba, kwenye kambi ya muda ya raia waliokimbia mapigano baina ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Al Houthi, tukio ambalo limesababisha darzeni kadha za vifo vya wahamiaji hawo wa ndani ya nchi.

WHO imekaribisha kwa mikono miwili misaada ya dawa kinga dhidi ya H1N1 kutoka mataifa tisa

Mataifa ya Marekani, Australia, Brazil, Ufaransa, Utaliana, New Zealand, pamoja na Norway, pamoja na Usweden na Uingereza yameripotiwa kuchangisha msaada wa dawa ya chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya A/H1N1, mchango ambao utasaidia pakubwa kuhudumia umma wa kimataifa.

Upungufu wa fedha utailazimisha WFP kupunguza chakula kwa wahitaji Kenya

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba kwa sababu ya upungufu wa misaada ya fedha kutoka wahisani wa kimataifa, litalazimika kupunguza posho ya chakula wanaofadhiliwa mamilioni ya raia wanaohitajia misaada ya dharura ya chakula nchini Kenya,

Hapa na pale

Ijumaa kumetolewa rasmi ripoti mpya ya KM juu ya watoto walionaswa kwenye mazingira ya mapigano nchini Burundi. Alisema kuanzia Agosti 2009 UM umethibitisha kutogundua tena watoto wa umri mdogo walioshirikishwa mapigano na majeshi ya mgambo katika Burundi. Alitilia mkazo kwenye ripoti kwamba jambo muhimu la kufanyika kwa sasa hivi ni kuhakikisha watoto wote waliohusikana na makundi yenye silaha katika siku za nyuma huwa wanajumuishwa kwenye kadhia za maisha ya kikawaida kwenye jamii zao. Ripoti imependekeza kuanzishwe mfumo mpya wa kuwalinda watoto, kwa ujumla, na hatari ya kuajiriwa kimabavu na makundi ya waasi. Vile vile KM alipendekeza ndani ya ripoti kwa Kundi la Kazi la Baraza la Usalama juu ya hifadhi ya watoto kwenye maeneo ya mapigano kuzuru Burundi katika miezi ijayo, ili kufuatilia maendeleo kwenye jitihadi za kutekeleza ile miradi ya kuwahifadhi watoto Burundi.

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imetangaza kushtushwa sana na kutishwa na idadi ya vifo vilivyosajiliwa katika eneo la uhasama la Yemen. UNHCR imeshapeleka mahema zaidi, magodoro na mablangeti kwa wahamiaji 2,000 ziada waliomiminikia kwenye eneo jirani la Saudi Arabia kutafuta hifadhi. Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya taarifa ilizopokea zinazosema mashambulio ya anga yaliofanyika karibuni kwenye kambi za wahamiaji wa ndani katika Yemen kaskazini, yalisababisha vifo kadha vya raia, ikijumlisha watoto wadogo. UNICEF ilisema hali hiyo ni msiba mkubwa katika Yemen kaskazini, hususan kwa watoto wadogo ambao mwezi mmoja tangu mapigano kufumka bado hawana fursa ya kupatiwa maji safi na salama, wala mazingira yanayoridhisha au utunzaji wa afya na hifadhi wanayostahiki.

UNCTAD inasema FDI kwa 2009 inaendelea kupungua kimataifa

Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) limewasilisha, kutoka Geneva, Alkhamisi ripoti yake mpya iliozingatia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kimataifa.