Habari Mpya

Namibia kuyasihi Mataifa Wanachama kupitisha hatua kali dhidi ya serikali zinazochukua madaraka kimabavu

Majadiliano ya wawakilishi wote bado yanaendelea kwenye ukumbi wa Baraza Kuu na yameingia siku ya sita hii leo.

Matayarisho ya mkutano wa Copenhagen yanavuta kasi Bangkok

Wajumbe wa kimataifa wanaokutana kwa sasa mjini Bangkok, Thailand Ijumatatu walianzisha majadiliano yanayokaribia duru ya mwisho ya maandalizi ya mkutano mkuu ujao wa Copenhagen,

Utata wa kwenye mapigano ya kisiku hizi unakwamisha huduma za UNHCR, anasema Guterres

Kwenye hotuba ya ufunguzi wa kikao cha 60 cha bodi la utawala la Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), Kamishna Mkuu wa Taasisi hiyo, Antonio Guterres, alisema kuongezeka kwa mizozo na vurugu yenye utata, isiowahi kushuhudiwa katika miaka iliopita, hali hiyo imezusha mazingira yenye kuhatarisha zaidi zile juhudi za mashirika ya UM za kuokoa maisha na kunusuru waathirika wa

Hapa na pale

Tume ya Kuchunguza Ukweli juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza inatazamiwa kuwakilisha ripoti ya matokeo ya ziara ya uchunguzi wao, mbele ya wajumbe wa Baraza la Haki za Binadamu, Ijumanne asubuhi, mjini Geneva. Ripoti itawakilishwa na kiongozi wa tume, Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini. Wajumbe watatu wengine wa tume wataungana na Jaji Goldstone kuwasilisha ripoti yao, ikijumlisha Bi Hina Jilani, Profesa Christine Chinkin na Kanali Desmond Travers. Kadhalika, Baraza la Haki za Binadamu litasikia ripoti nyengine juu ya Ghaza kutoka Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, ikifuatiwa na taarifa za wawakilishi wa Falastina na Israel. Mswada wa azimio la kikaohicho umeshatayarishwa na Baraza la Haki za Binadamu, na utazingatiwa kupitishwa Alkhamisi au Ijumaa.

Kilimo katika Afrika kinaashiria maendeleo ya kuridhisha, inasema FAO

Ripoti ya makala ya kujadiliwa, iliochapishwa hii leo na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza kwamba utendaji hakika, wa kutia moyo, ulioshuhudiwa kufanyika hivi karibuni kwenye sekta ya kilimo katika zile nchi za Afrika ziliopo kusini ya eneo la Jangwa la Sahara, umebainisha utengano halisi na tabia za kikale, zilizopitwa na wakati, za kilimo, na kuwakilisha mwelekeo mpya wenye matarajio ya ukuzaji kilimo maridhawa kieneo, maendeleo yatakayokuwa na natija kubwa kwa umma, kwa ujumla.

Baraza Kuu laanzisha tena majadiliano ya jumla ya mataifa wanachama

Majadiliano ya jumla kwenye kikao cha mwaka cha wawakilishi wote, yameanza tena rasmi leo asubuhi hapa kwenye Makao Makuu, kufuatia kikao cha siku nzima cha Baraza Kuu kilichokusanyika Ijumamosi, ambapo wazungumzaji waliowakilisha mataifa 30 waliwakilisha hoja kadha wa kadha kuhusu taratibu wa kusuluhisha masuala yenye kusumbua umma wa kimataifa.

Ripoti juu ya Ushirikiano wa Viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA)

Kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la UM, ambacho ni cha 64, kilianza rasmi wiki hii kwenye Makao Makuu. Viongozi wa Mataifa na Serikali zaidi ya 120 walikusanyika mjini New York kuhudhuria mikutano mbalimbali juu ya shughuli za usalama, amani, haki za binadamu, huduma za maendeleo na kadhalika.

FAO imeripoti kuwa uwekezaji kwenye utafiti wa kilimo ni muhimu kwa maendeleo

Ripoti iliochapishwa hii leo na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza Mataifa Wanachama yatahitajia kuwekeza, kwa kiwango kikubwa zaidi, kwenye shughuli za utafiti ambao matokeo yake yatayawezesha mataifa, hasa zile nchi masikini, kutumia teknolojia mpya ya ukulima na kwenye matumizi ya mazao makuu tofauti yatakayosaidia kuzalisha mavuno kwa wingi zaidi.

OCHA inasema hali Yemen Kaskazini inazidi kuwa mbaya

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali katika jimbo la Kaskazini la Yemen, la Sa\'ada, na katika maeneo jirani, inaendelea kuharibika kwa sababu ya kushtadi kwa mapigano baina ya vikosi vya usalama vya Yemen na makundi ya wapinzani ya Al Houthi.

WHO yatangaza taarifa mpya ya dawa ya kuzuia virusi vya A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba uzoefu uliopatikana kimataifa kwenye huduma za kutibu janga la homa ya mafua ya A/H1N1 umethibitisha umuhimu kwa mgonjwa kupata matibabu ya mapema kwa kutumia zile dawa za kupambana na virusi vya maradhi, zinazoitwa oseltamivir na zanamivir,