Habari Mpya

Kikao cha 53 cha IAEA chafunguliwa rasmi Vienna

Kikao cha 53 cha Baraza Kuu la la Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) kimeanza rasmi Ijumatatu mjini Vienna, Austria na kwenye risala ya ufunguzi KM alitilia mkazo ulazima wa kuwa na mfumo unaoridhisha utakaohakikisha udhibiti bora wa silaha za kinyuklia, na kuhakikisha hazitoenezwa kimataifa.

Wakulima wa Zimbabwe wasaidiwa na FAO kuotesha mahindi na mtama

Katika jitihadi za kuisaidia Zimbabwe kukabiliana na tatizo la njaa kwa mwaka huu, Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), likishirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) yatawapatia mbegu na mbolea baina ya asilimia 10 hadi 15 ya wakulima dhaifu nchini, sawa na wakulima 176,000.

Mafuriko makali Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 ziada

Imeripotiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ya kwamba mafuriko makali ya karibuni Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 hivi sasa na kusababisha vifo 159.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon, Ijumatatu, kwenye mkesha wa ufunguzi wa kikao cha 64 cha Baraza Kuu la UM, tarehe 14 Septemba, alijiunga kwenye sala maalumu ya kuomba dua ya mafanikio na amani ulimwenguni. Sala hii kawaida hufanyika kwenye Kanisa la Familia Takatifu (Holy Family Church) kila mwaka kabla ya ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu, ambacho huhudhuriwa na viongozi kutoka nchi zote za dunia na hufanyika kwenye Makao Makuu ya UM kujadiliwa kipamoja miradi ya kuimarisha usalama na amani ya kimataifa. KM alikumbusha kwenye risala yake kwamba wakati UM ukijaribu kuzisaidia nchi maskini kukamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), haitoweza kuponesha majeraha ya zile ahli za kimataifa zinazosumbuliwa na shida na matatizo ya kiuchumi. Alitoa mwito maalumu kwa viongozi wote wa makundi ya kidini kujitahidi kuungana ili kuimarisha ule uwezo wa kuyatekeleza malengo ya UM ya kunusuru maisha ya umma, na kuusaidia ulimwengu kuelekea kwenye hali nzuri ya kuusaidia umma, kwa ujumla.

UNHCR kupongeza miaka 40 ya mkataba wa kihistoria Afrika kuhifadhi wahamiaji

Alkhamisi ya tarehe 10 Septemba iliadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa mkataba wa mataifa ya Afrika kuhifadhi wahamiaji.

UNESCO imemteua Paul Ahyi wa Togo kuwa msanii mpya wa kutetea amani

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Alkhamisi limemteua msanii wa kutoka Togo, anayeitwa Paul Ahyi kuwa mwanachama mpya wa orodha ya watu mashuhuri wanaotumia sauti zao, vipaji na hadhi walizonazo kusaidia kutangaza ujumbe wa UNESCO ulimwenguni, na kuendeleza miradi ya taasisi hii ya UM kimataifa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Usomali azuru Somaliland

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah Alkhamisi alizuru Somaliland ambapo alipata fursa ya kukutana na viongozi wa huko kwa majadiliano kuhusu mpango wa amani na mfumo wa uchaguzi kwenye eneo, pamoja na kusailia masuala kadha mengine muhimu.

Taarifa za sasa za WHO juu ya kupunguza homa ya A/H1N1 kwenye maskuli

Shirika la Afya Duniani (WHO) Ijumaa limetangaza nasaha maalumu kuhusu hatua za kuchukuliwa katika maskuli, ili kupunguza athari za janga la homa ya mafua ya H1N1.

Hapa na pale

David Gressly, Mratibu wa Eneo la Sudan Kusini kwa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan (UNMIS) Ijumaa alizungumza na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, kwa kupitia njia ya vidio, ambapo alieleza ya kuwa mashambulio ya kikatili yanayoendelezwa na kundi la waasi wa Uganda wa LRA pamoja na miripuko ya karibuni ya mapigano ya kikabila ni mambo yanayohatarisha usalama wa umma wa Sudan kusini. Alizungumzia kutoka Sudan kusini na alieleza wanajeshi wa mgambo wa LRA, ambao huteka nyara watoto wadogo na huwatumia kama wapiganaji na watumwa wa kikahaba, wameselelea na kuendelea kuongoza operesheni zao kwenye eneo la magharibi ya mbali ya Sudan kusini. Kwenye jimbo la Western Equatoria kundi la LRA linaendelea na kampeni zao za vitisho - ambapo huiba mali na kuvamia nyumba za watu, makanisa na vituo vya afya. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) waasi wa Uganda wa LRA wameonekana wakoiba vyakula, na kuua raia wasio hatia, na vile vile huwateka nyara watoto wadogo wa kike na kiume ambao huwalazimisha kuwatumikia kwa nji zinazoharamisha kabisa kanuni za kiutu na haki za mtoto. Gressly alitoa mfano wa uharibifu wa waasi wa LRA, ambao katika mwezi Agosti mwaka huu walishammbulia maeneo ya Western Equatoria na Central Equatoria na kuzusha tatizo kubwa la watu 80,000 ziada kung\'olewa mastakimu. Kuhusu mapigano miongoni mwa makabila ya Sudan kusini, Gressly alibainisha kwamba mara nyingi uhasama baina yao hutokana na mabishano ya mali - hususan ngo\'mbe, maji na ardhi. Alisisitiza kwamba suala la umiliki wa ardhi ni "tatizo kubwa linalohitajia suluhu ya kuridhisha miongoni mwa makabila ya eneo la kusini, au si hivyo fujo na vurugu zitaendelea kusababisha hali ya hatari na wasiwasi Sudan kusini."

Mwathirika wa mateso ya vita katika JKK azungumzia maafa aliopata na msaada anaotoa kihali kwa waathirika wengine

Mnamo mwanzo wa mwezi Septemba UM uliwakilisha ripoti mbili muhimu, zilizochapishwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu na pia kutoka Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC).