Habari Mpya

Mashambulio ya kikabila Sudan Kusini yalaaniwa na KM

KM ameshtumu vikali shambulio liliotukia mwisho wa wiki liopita katika Sudan kusini, ambapo iliripotiwa watu 100 ziada waliripotiwa kuuawa, ikiwa miongoni mwa msururu wa mapigano ya kikabila yaliopamba karibuni kwenye eneo hili la Sudan.

Kesi ya waziri aliyetuhumiwa makosa ya jinai ya halaiki Rwanda yaanza kusikilizwa na ICTR

Kesi ya aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Maendeleo katika Rwanda, yaani Augustin Ngirabatware, imeanza kusikilizwa rasmi leo Ijumatano kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR).

Suluhu ya wahusika wengi ndio inayohitajika kutatua mizozo ya kimataifa, asihi Raisi wa BK

Raisi wa Baraza Kuu (BK), Ali Treiki wa Libya, kwenye risala yake ya ufunguzi wa majadiliano ya jumla, aliyahimiza Mataifa Wanachama kushirikiana, kwa ukaribu zaidi, na taasisi ya UM.

Kikao cha 64 cha Baraza Kuu kufunguliwa rasmi

Viongozi wa dunia 120 ziada, waliokusanyika kwenye Makao Makuu asubuhi ya leo, wameanza rasmi, majadiliano ya jumla ya kila mwaka, kwenye kikao cha wawakilishi wote katika ukumbi wa Baraza Kuu la UM, siku moja baada ya kumalizika Mkutano Mkuu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

VVU/UKIMWI vinahatarisha usalama na amani ya kimataifa

Ripoti mpya iliotolewa bia leo hii na Baraza la Utafiti wa Sayansi ya Jamii, New York, Marekani pamoja na Tassisi ya Clingendael juu ya Uhusiano wa Kimataifa iliopo mji wa Hague, Uholanzi imethibitisha hatari anuwai ya virusi vya UKIMWI katika usalama na amani ya kitaifa na kimataifa.

FAO inasema njaa imekithiri Afrika Mashariki

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kwamba hali mbaya ya ukosefu wa chakula katika eneo la Pembe ya Afrika itayalazimisha mashirika ya kimataifa kukithirisha mchango wao wa chakula, kwa umma muhitaji wa eneo, umma ambao idadi yao inaendelea kukithiri.

Kampeni ya kupandisha miti bilioni duniani ilifanikiwa kupita kiasi, imeripoti UNEP

Imetangazwa hii leo kwamba ile kampeni ya kimataifa ya kuotesha miti bilioni moja katika ulimwengu, kwa madhumuni ya kujikinga na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa, imefanikiwa kufikia kiwango kilichokiuka matarajio ya waandalizi wa mradi huo.

Mataifa ya Visiwa Vidogo yakumbusha jamii ya kimataifa dhamana yao

Mataifa Yanayoendelea ya Visiwa Vidogo yanayowakilisha nchi 42 yametoa mwito maalumu wenye kusisitiza maafikiano ya kimataifa ya 2012 juu ya hali ya hewa, yatawajibika kudhaminia uwezo wa nchi maskini sana kupata riziki,

Mkutano Mkuu juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Kwenye Mkutano wa UM juu ya Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa, unaofanyika hapa Makao Makuu, KM Ban Ki-moon aliwahimiza wakuu wa Taifa na serikali 100, waliohudhuria kikao hicho kuharakisha, kwa vitendo, zile hatua za kudhibiti bora tatizo la kuongezeka kwa hali ya joto ulimwenguni ili kuihifadhi sayari yetu kwa vizazi vijavyo.

Hapa na pale

KM ameikaribisha hatua iliochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Kideomkrasia ya Kongo, mnamo tarehe 20 Septemba, ya kumpeleka Grégoire Ndahimana kizuizini Tanzania, kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda. Ndahimana, raia wa Rwanda aliyekuwa na cheo cha juu kwenye kundi la waasi wa Rwanda la FDLR, alikamatwa na vikosi vya JKK mnamo tarehe 10 Agosti 2009 kwenye jimbo la mashariki ya nchi. Alikuwa miongoni mwa watoro 13 walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kuharamisha sheria za kiutu za kimataifa nchini Rwanda katika 1994. Kutiwa mbaroni Ndahimana na uhamisho wake kwenye Mahakama ya ICTR ni vitendo vilivyosaidiwa kwa mchango wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC), baada ya kuitika ombi la wenye mamlaka nchini humo.