Habari Mpya

Malaria Kenya imepunguzwa na mchanganyiko wa tiba mpya

Taarifa ya jarida linalochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) liliotolewa kwa mwezi Septemba, limebainisha ya kuwa tiba mpya iliovumbuliwa, ya mchanganyiko, ina uwezo wa kupunguza kwa kiwango kikubwa hatari ya maambukizo ya malaria kwa watoto wadogo.

Uwekezaji wa katika mifumo ya ikolojia una matumaini ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, inasema TEEB

Matokeo ya mradi ulioanzishwa na Ujerumani pamoja na Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya kuhusu masuala ya hali ya hewa, unaosimamiwa na Taasisi juu ya Uchumi wa Mfumo wa Ikolojia na Viumbe Hai Anuwai (TEEB), yamethibitisha dhahiri kwamba uwekezaji kwenye huduma za kufufua mifumo ya ikolojia ni hatua yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, na ni hatua itakayoimarisha uchumi wa kimataifa, halkadhalika, pindi itatekelezwa kama inavyostahiki.

KM ahimiza mataifa kukamilisha maafikiano ya Mkutano Mkuu juu ya taathira za hali ya hewa

KM Ban Ki-moon amewasihi walimwengu kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana haraka na athari chafuzi za mabadiliko ya hali ya hewa, na kuyahifadhi maisha ya vizazi vijavyo.

Hapa na Pale

KM Ban Ki-moon leo alizuru Mzingo wa Barafu wa Ncha ya Dunia (Polar Ice Rim) wakati alipokuwa ndani ya meli ya Norway. Kabla ya hapo KM na mkewe walizuru Steshini ya Zeppelin, kituo cha Norway kiliopo Kaskazini ya dunia, kunapoendelezwa uchunguzi wa hewa ya eneo la Akitiki, utafiti ambao hufuatilia athari za hewa chafu inayomwagwa angani pamoja na vichafuzi vyengine. KM alipata fursa ya kujionea binafsi majabali ya barafu yalionywea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, hali ambayo alisema ilimshtusha sana. Ilivyokuwa chini ya siku 100 zimesalia kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu wa Copenhagen juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa, KM alisema safari yake ya kaskazini ya ncha ya dunia imempatia fursa ya kujionea mwenyewe athari za mazingira, hali itakayomsaidia kuwahamasisha wajumbe watakaohudhuria Mkutano wa Copenhagen juu ya dharura ya kukamilisha mapatano ya mkataba mpya wa kuhifadhi mazingira, na kudhibiti bora athari chafuzi zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mwanajeshi wa Rwanda akabidhiwa madaraka ya Kamanda Mkuu mpya kwa Darfur

Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) kutoka Rwanda, Liuteni-Jenerali Patrick Nyamvumba ameripotiwa kuanza kazi rasmi hii leo.

Maharamia wa uvuvi watanyimwa makimbilio salama baada ya kufikiwa maafikiano mapya ya kimataifa

Mataifa Wanachama 91 wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) yameafikiana kuukubali waraka wa mwisho wa mkataba wa kimataifa uliokusudiwa kupiga vita uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

OHCHR imepeleka timu ya wataalamu wa haki za binadamu Gabon kufuatilia uchaguzi wa uraisi

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR) imetuma wataalamu wanne nchini Gabon, kuchunguza hali ya haki za binadamu, kwa ujumla, wakati uchaguzi wa uraisi unapofanyika katika taifa hili la Afrika Magharibi.

UNHCR yahadharisha, mzozo mkuu wa kiutu wajiandaa kuripuka Yemen kaskazini

UM unaashiria mzozo mkubwa wa kiutu unajiandaa kufumka katika mji wa Sa\'ada, uliopo Yemen kaskazini, ambapo hali huko inaripotiwa kila siku kuendelea kuporomoka na kuharibika.

Mapigano makali Mogadishu yanaathiri zaidi raia, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kutoka Geneva kwamba mapigano makali yaliopamba kwenye mji wa Mogadishu, Usomali yanaendelea kuathiri kwa wingi raia.