Habari Mpya

UNAMID imekamilisha thuluthi mbili ya maofisa wa polisi wanaohitajika kulinda raia

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) leo limeripoti kuwasili kwenye mji wa El Fasher, wiki hii, maofisa wa polisi 130 watakaotumiwa kuimarisha usalama kwenye kambi za wahamiaji wa ndani ya nchi.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anataka kufanyike uchunguzi wa haraka Guinea juu ya mauaji ya kihorera ya karibuni

Kamishna Mkuu wa UM kuhusu Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa mwito wa kubuniwa tume maalumu ya uchunguzi, itakayopelekwa Guinea, kutathminia ripoti inayoeleza Ijumatatu vikosi vya usalama vya Guinea viliua kihorera raia walioandamana mjini Conakry, waliowakilisha kundi la upinzani.

Baraza la Usalama kupendekeza UM uwe na Mjumbe Maalumu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsiya

Baraza la Usalama lilkutana Ijumatano kuzingatia suala la hifadhi ya raia dhidi ya vitendo vyote vya kutumia mabavu na unyanyasji wa kijinsia, kwenye mazingira ya mapigano, hususan kwa raia wanawake na watoto wadogo.

Wagonjwa milioni nne wenye VVU wamefanikiwa sasa hivi kupatiwa tiba ya ART, kurefusha maisha

Kuanzia mwisho wa 2008, watu milioni 4 wanaoishi kwenye nchi zenye pato la chini na la wastani, walioambukizwa virusi vya UKIMWI, walifanikiwa kupata zile dawa za matibabu za kurefusha maisha za ART. Jumla hii inawakilisha ongezeko la asilimia 36, kwa mwaka, la wagonjwa wanaotibiwa kwa dawa ya ART.

Raisi wa BK anatabiri 'enzi mpya ya uhusiano wa kimataifa' wakati wa kufunga majadiliano ya wawakilishi wote

Ijumanne mchana Baraza Kuu la UM lilikamilisha wiki moja ya majadiliano ya mwaka ya wawakilishi wote, ambapo wajumbe kutoka nchi 192 walizungumza, ikijumlisha Wakuu wa Mataifa na Serikali 107, waliowasilisha hoja kadha juu ya sera za kuendeleza uhusiano wa kimataifa.

Hapa na Pale

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) limekaribisha amri ya utendaji iliotangazwa na Raisi Omar al-Bashir wa Sudan kusimamisha, haraka, zile sheria za ukaguzi na uchunguzi wa magazeti katika nchi. UNMIS iliripoti pindi uamuzi huo utatekelezwa utasaidia kuendeleza na kuimarisha mapendekezo ya Mapatano ya Amani ya Jumla (CPA) baina ya eneo la kaskazini na kusini, na kuandaa mazingira bora ya kutayarisha uchaguzi wa vyama vyingi uliopangwa kufanyika Aprili 2010.

KM ameridhika na mahojiano ya awali kwenye kikao cha mwaka cha BK

KM Ban Ki-moon alifanya mahojianio na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, leo asubuhi, na aliwaambia wanahabari kwamba maendeleo makubwa yalipatikana tangu kikao cha 64 cha Baraza Kuu (BK) kuanza rasmi wiki iliopita, ambapo viongozi wa dunia walifikia maafikiano kadha kwenye juhudi zao za kutafuta suluhu ya kuridhisha ya masuala makuu yanayotatanisha ulimwengu wetu, ikijumlisha udhibiti wa madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukomeshaji wa silaha za maangamizi za kinyuklia na kwenye mizozo ya kifedha katika soko la kimataifa.

UNAMID imelaani shambulio la Darfur Magharibi dhidi ya wafanyakazi raia na wanajeshi

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limelaani vikali shambulio dhidi ya moja ya msafara wao wa ulinzi, liliotukia Ijumatatu usiku kwenye mji wa El Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa ulinzi amani.

WFP/Taasisi ya Mradi wa Vijiji vya Milenia zaungana kupunguza wenye njaa na utapiamlo Afrika

Kadhalika, mapema wiki hii Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), likijumuika na mpango wa maendeleo unaoungwa mkono na UM, unaoitwa Mradi wa Vijiji vya Milenia, yameanzisha bia mradi mwengine mpya unaojulikana kama mradi wa "maeneo huru dhidi ya ukosefu wa chakula cha kutosha" utakaotekelezewa vijiji 80 katika nchi 10 za Afrika, kusini ya eneo la Sahara.

Ukame katika Uganda unaitia wasiwasi WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti rasmi hii leo kuingiwa wasiwasi kuhusu mfululizo wa mvua haba katika Uganda kwenye majira ya mvua, hali iliosababisha watu milioni mbili kukosa uwezo wa kupata chakula na kuomba wasaidiwe chakula na mashirika ya kimataifa kunusuru maisha.