Habari Mpya

Taarifa rekibisho ya maambuziki ya A/H1N1 kutoka WHO

[Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti Ijumaa, kutokea Geneva kwamba maambukizi ya homa ya mafua ya A/H1N1 bado yanaendelea kimataifa, hali ambayo imeshasababisha vifo vya wagonjwa 800 katika nchi 160 duniani, zilizoripoti kugundua maambukizi ya maradhi haya kwenye maeneo yao.

Ban anaamini miradi ya kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa Uchina inaweza kurudiwa kimataifa

KM Ban Ki-moon, ambaye anafanya ziara ya siku nne katika Uchina, Ijumaa alihudhuria mjini Beijing, tukio la kuanzisha mradi bia wa UM na Serikali ya Uchina kuhimiza umma wa huko, kutumia ile balbu ya taa yenye kuhifadhi nishati na inayotumika kwa muda mrefu.

Suluhu ya kikanda Afrika ndio yenye uwezo wa kukomesha mizozo, inasema BK

Baraza Kuu (BK) Alkhamisi limepitisha, bila kupingwa, azimio liliobainisha umuhimu wa kutumia utaratibu wa kikanda kuzuia na kusuluhisha mizozo katika bara la Afrika.

Msomi wa Kenya, Ngugi wa Thiong'o, ajumuisha maoni binafsi juu ya 'wajibu wa kimataifa kulinda pamoja raia'

Alkhamisi asubuhi, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kisio rasmi, walikusanyika wataalamu wa kimataifa walioshiriki kwenye majadiliano yenye hamasa kuu, kuzingatia ile rai ya miaka ya nyuma ya kukomesha kile kilichotafsiriwa na wajumbe wa UM kama ni "kiharusi cha kimataifa" katika kukabili maovu na ukatili unaofanyiwa raia, ndani ya taifa, wakati wenye mamlaka wanaposhindwa kuwapatia raia hawa ulinzi na hifadhi wanayostahiki.

Maelfu ya raia wang'olewa makazi na mapigano Kivu Kaskazini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti hali ya machafuko yaliozuka karibuni kwenye Jimbo la Kivu Kusini, katika sehemu ya mashariki ya JKK imesababisha watu 35,000 kung\'olewa makazi, hasa kwenye lile eneo la uwanda tambarare la Mto Ruzizi, ambapo JKK hupakana na nchi jirani za Burundi na Rwanda.

Hapa na pale

Kamati ya UM ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) ambayo inakutana wiki hii kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, imeanza shughuli za kusailia namna nchi wanachama zinavyotekeleza mikataba ya kimataifa ya kukomesha ubaguzi wa kijinsiya. Kamati hii ya CEDAW imetimia miaka 30 katika mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake, Naela Mohammed Gabr wa kutoka Misri, Ijumatano aliwaambia waandishi habari wa Makao Makuu kwamba miongoni mwa masuala muhimu wanayoyazingatia kwenye kikao cha safari hii ni pamoja na ile mada inayohusu taathira za mizozo ya fedha iliopamba duniani karibuni na namna inavyochafua huduma za kimsingi za jamii. Vile vile alisema Kamati inasailia mada zinazohusu mishahara wanaopatiwa wanawake kwenye mazingira ya mizozo ya kifedha kimataifa, pamoja na tatizo la kuzidi kwa ukosefu wa kazi miongoni mwa wanawake." Kwa mujibu wa taarifa za UM Kamati ya CEDAW hutumia taratibu mbalimbali za kuhamasisha nchi wanachama kutekeleza mapendekezo yake ya kukomesha ubaguzi wa kijinsiya, mathakan, Kamati mara nyingi huchapisha rasmi ukiukaji wa haki za wanawake katika taifa fulani, fafanuzi ambazo baadaye huutumiwa Ofisi ya Kamisheni wa UM juu ya Haki za Binadamu iliopo Geneva. Ofisi ya haki za Binadamu hujumuisha matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya CEDAW kwenye ule Mradi wa Mapitio ya Jumla kuhusu namna haki za binadamau zinavyotekelezwa katika Mataifa Wanachama 192 wa UM. Mapitio haya hufanyiwa kila taifa, mara moja katika kila miaka minne. Kwenye mkutano wa wiki hii wataalamu 22 wa Kamati ya CEDAW wanafanyia mapitio juu ya hali za wanawake katika mataifa ya Azerbaijan, Bhutan, Denmark, Guinea-Bissau, Laos, Ujapani, Liberia na pia Uspeni, Uswiss, Timor-Leste na Tuvalu.

Ethiopia kufadhiliwa msaada wa dharura na CERF

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, Alkhamisi imetangaza kutoka Geneva ya kuwa itaifadhilia Ethiopia msaada wa dola milioni 6,

FAO imeanzisha huduma ya pamoja kupiga vita Ugonjwa wa Midomo na Miguu unaoambukiza wanyama

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limeanzisha operesheni mpya za kupambana na tatizo la kusambaa kwa Ugonjwa wa Midomo na Miguu wenye kuambukiza wanyama.

Ripoti ya KM juu ya hali Usomali

Ripoti ya KM juu ya Usomali leo imewakilishwa rasmi hapa Makao Makuu. Ndani ya ripoti, KM alibainisha wasiwasi mkubwa alionao kuhusu majaribio ya karibuni ya makundi ya upinzani ya kutaka kupindua, kwa kutumia nguvu, serikali halali ya Usomali.

Uwajibikaji wa taifa kulinda raia ni wazo linaloungwa mkono na Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu iliochangisha maoni ziada kuhusu mjadala unaofanyika wiki hii, hapa Makao Makuu, kuzingatia suala la "Wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa Kulinda Raia".