Habari Mpya

Watoto waliopo vizuizini Rwanda kusaidiwa mawakili na mradi wa UM

Kadhalika Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba linaunga mkono, na kuahidi pia kuusaidia ule mradi ulioanzishwa na Wizara ya Utawala wa Sheria ya Rwanda, wa kuwapatia watoto 600 ziada waliomo vizuizini, mawakili wa kuwatetea kesi zao.

UM kuisaidia Angola kuhudumia raia maji safi

Mradi wa Pamoja wa Mashirika ya UM Kuhudumia Maji na Usafi umeanzishwa rasmi karibuni nchini Angola.

Hapa na pale

Ripoti mpya ya KM kuhusu maandalizi ya uchaguzi katika Sudan, uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwezi Aprili 2010, imeeleza kwamba ijapokuwa kumepatikana mafanikio ya kutia moyo kwenye matayarisho ya jumla, hata hivyo, hatua chache za kimsingi zimesalia kutekelezwa na Serikali ya Sudan. Ripoti ilionyesha kuna ukosefu wa kudhaminia kihakika haki za kimsingi kwa raia wakati wa kupiga kura, ikijumlisha uhuru wa kukusanyika, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kusema, ikiwa miongoni mwa masuala kadha ambayo yameyafanya baadhi ya mashirika ya kiraia kutokuwa na imani kuhusu uchaguzi ujao. KM ameisihi Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan kuchukua hatua halisi zitakazohakikisha raia wote waliong\'olewa makazi pamoja na wahamiaji, na wale waliokosa vitambulisho, huwa wanajumuishwa kwenye miradi ya uchaguzi. KM alisema UM upo tayari kutekeleza mpango wa awamu mbili utakaotumiwa kuzisaidia kamisheni 25 za uchaguzi katika majimbo, kwa kusafirisha vifaa vye kuendesha uchaguzi kama inavyotakikana kisheria.

Mkutano wa 'R2P' wahitimisha mijadala kwenye Baraza Kuu

Baraza Kuu la UM Ijumanne alasiri limekamilisha mahojiano kuhusu lile suala la ‘dhamana ya Mataifa kulinda raia dhidi ya jinai ya halaiki", rai ambayo vile vile hujulikana kwa umaarufu kama ‘kanuni ya R2P.\'

Mjumbe wa UM kwa Usomali asema msaada wa jumuia ya kimataifa unahitajika kidharura kurudisha utulivu nchini

Baraza la Usalama lilikutana leo asubuhi kuzingatia hali katika Usomali. Risala ya ufunguzi ya Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Oul-Abdallah iliwahimiza wajumbe wa Baraza kuchukua "hatua thabiti" zitakazosaidia kurudisha tena utulivu kwenye taifa hili la Pembe ya Afrika, hasa katika kipindi cha sasa ambapo mapigano ndio yameshtadi zaidi kati ya majeshi ya mgambo wapinzani ya Al-Shabaab na Hizb-al-Islam dhidi ya vikosi vya Serikali, uhasama ambao ulizuka tena upya mjini Mogadishu mnamo tarehe 07 Mei (2009).

KM ameshtushwa na mapambano ya kimadhehebu Nigeria Kaskazini

Kadhalika, Ijumanne, KM alitoa taarifa maalumu yenye kuelezea wasiwasi wake mkuu juu ya ripoti za kuzuka, hivi majuzi, duru nyengine ya mapigano ya kimadhehebu katika Nigeria kaskazini, vurugu ambalo limesababisha korja ya vifo.

Ban anasema ni muhimu kwa Mataifa kuhitimisha mashauriano ya mkataba wa kudhibiti hali ya hewa

KM Ban Ki-moon leo alikuwa na mazungumzo ya kila mwezi na waandishi habari wa kimataifa waliopo hapa Makao Makuu ya UM. Kwenye taarifa ya ufunguzi KM alizingatia zaidi suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni na juhudi za kimataifa za kulidhibiti tatizo hili.

Baraza la Usalama lasailia hali ya usalama katika Chad/JAK

Baraza la Usalama asubuhi lilifanyisha kikao cha hadhara kusailia hali ya usalama katika Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK). Mjumbe Maalumu wa KM anayeshughulikia huduma za ulinzi amani wa mataifa haya mawili, Victor Angelo, alipowakilisha taarifa yake mbele ya Baraza alisema jumuiya ya kimataifa inawajibika kuharakisha kufanyika majadiliano ya kidiplomasiya ili kurudisha utulivu na amani ya eneo, kufuatilia mapigano yalioripuka karibuni baina ya Chad na Sudan.

Maambukizi ya A/H1N1 ni ya wastani kwa sasa, inasema WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo hii kwamba maambukizi ya janga la homa ya mafua ya A/H1N1 kimataifa yanakadiriwa kuwa bado ni ya wastani, na wingi wa watu wanaouguwa maradhi haya kwa sasa, kwa bahati, hawashuhudii maumivu makali na hawahitajiki kulazwa hospitali.

Watu milioni 6.2 Ethiopia wanakabiliwa na hatari maututi ya utapiamlo, OCHA inahadharisha

Fidele Sarassoro, Mratibu wa Misaada ya Kiutu katika Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) ametangaza kwamba taifa la Ethiopia linakabiliwa kwa sasa na tatizo la kuhudumia mamilioni ya raia misaada ya kihali, kwa sababu ya upungufu wa chakula, huduma za afya, lishe bora pamoja na maji safi na usafi wa mazingira, ikichanganyika pia na matatizo ya ukosefu wa makazi ya dharura, ajira na ukosefu wa shughuli za kilimo ambazo zinahitajika kuwasaidia raia kupata riziki.