Habari Mpya

Tukio la mripuko Tanzania bado linaathiri kihali maelfu ya raia

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) imeripoti maelfu ya raia wa Tanzania waliong’olewa makazi, wiki tatu nyuma, kwenye eneo la Dar es Salaam liliopo karibu na kambi ya kijeshi, bado wanaendelea kuishi kwenye mazingira magumu na wanahitajia kufadhiliwa misaada ya dharura, ya kihali, kwa muda mrafu ujao, kumudu maisha.

Hali ya ukatili dhidi ya raia katika majimbo ya JKK kuitia wasiwasi UNHCR

Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), kutokea Geneva, amesema UM una wasiwasi na ripoti ilizopokea juu ya kuendelea kwa vitendo vya ukatili, ikichanganyika na matumizi mabaya ya mamlaka pamoja na unyanyasaji dhidi ya raia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini katika JKK.

Baraza la WHO lahitimisha mkutano wa mwaka Geneva

Mkutano wa mwaka wa Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO) umemaliza kikao cha 2009 Ijumaa ya leo, kikao ambacho Mkurugenzi wa WHO, Dktr Margaret Chan alisema kilifanikiwa kuwapatia walimwengu “bishara ya nguvu ya masharti ya kudumu kuhusu maamirisho ya miradi ya afya ya jamii” pote ulimwenguni.

Hapa na pale

Staffan de Mistura, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Iraq ameshtumu, kwa kauli kali, mashambulio ya mabomu yaliotukia Kirkuk leo Alkhamisi na yale mashambulio mengine yaliofanyika kwenye mji wa Baghdad hapo jana. De Mistura alisema vitendo hivi viliwakilisha "uhalifu uliolenga kihorera raia wa Iraq" na vikijumuisha "jinai ya kulaumiwa vikali" na jamii yote ya kimataifa. Mjumbe wa KM kwa Iraq aliwatumia, kwa masikitiko makubwa aila za wafiwa, mkono wa taazia, kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na vile vile aliwaombea waathiriwa majeruhi wapone haraka.

Nchi zinazoendelea zahitajia misaada maridhawa kuokoka na mizozo ya fedha, inashauri UM

UM umearifu ya kuwa fungu kubwa la mataifa yanayoendelea hivi sasa yanafanana na waathiriwa wasio hatia wa ile mizozo ya fedha iliopamba karibuni kwenye soko la kimataifa, wakati mataifa tajiri, yaliosababisha mzozo huo, hayajaonyesha dhamira ya kuzisaidia nchi maskini katu kukabiliana na mgogoro huu wa fedha.

Ripoti mpya ya UM juu ya JKK inalenga hali Kivu Kaskazini

Ripoti ya mwanzo ya Tume ya Wataalamu juu ya JKK kuhusu hali ya usalama katika jimbo la Kivu Kaskazini, imeelezea matatizo yaliozuka kwenye juhudi za kuchanganyisha wapiganaji wa majeshi ya mgambo, na jeshi la taifa la FARDC kuanzia kipindi cha mwisho wa 2008 hadi manzo wa 2009.

Utekaji nyara wa misaada ya kihali Usomali umelaumiwa vikali na UNICEF

Imetangazwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kuwa inalaani, kwa kauli kali, utekaji nyara pamoja na uharibifu wa misaada ya kiutu na majengo yake, ulioripotiwa kuendelezwa na majeshi ya mgambo kwenye mji wa Jowhar katika Usomali.

Vifo vya watoto wachanga vimeteremeka karibuni, imeripoti WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limewasilisha ripoti mpya ya maendeleo inayofungamana na zile juhudi za kuyatekeleza, kwa wakati, Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayohusu juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga ulimwenguni.

IGAD inaliomba BU kuweka vikwazo dhidi ya anga ya Usomali

Taasisi juu ya Maendeleo baina ya Serikali za Afrika Mashariki, (IGAD) imelitumia Baraza la Usalama (BU) ombi la kuitaka ipige marufuku ndege zote kuruka kwenye anga ya Usomali, kwa makusudio ya kuwanyima wale waliotambuliwa kama "wadhamini na wafadhili wa kigeni" fursa ya kupeleka silaha, marisasi na baruti nchini humo.

UM wajitayarisha kuhudumia waathirika wa ukama Kenya

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripotiwa wiki hii kuandaa operesheni za kuhudumia misaada ya kunusuru maisha ya watu milioni 3.5, walioathirika na mavuno haba, kutokana na mvua chache katika Kenya mashariki.