Habari Mpya

UM kupunguza wahudumia misaada ya kiutu katika Chad

UM umetangaza kwamba kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuharibika katika eneo la Chad ya mashariki zile huduma za kupeleka misaada ya kihali kwa wahamiaji wa Sudan 110,000 waliopo huko zitabidi zipunguzwe pamoja na kupunguza wafanyakazi wa UM wanaohusika na kadhia hizo.

Jumuiya ya Kimataifa Yaadhimisha 'Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani'

Mnamo 1988 Baraza Kuu la UM lilitoa mwito maalumu uliopendekeza kuutekeleza uamuzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa kuifanya tarehe 01 Disemba kila mwaka kuwa ni ‘Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani.’

Mapigano makali Sudan ya kusini yaharamisha maafikiano ya amani, ashtumu KM

KM Kofi Annan ameripotiwa kushtumu yale mapigano makali yalioshtadi hivi majuzi katika mji wa Malakal, uliopo katika Jimbo la Nile ya Juu, Sudan ya Kusini, uhasama uliozuka kati ya Jeshi la Serekali ya Sudan (SAF) na kundi la waasi la SPLA. Kitendo hiki, alisisitiza KM, kiliharamisha kihakika na kukiuka yale Maafikiano ya Jumla ya Amani.

Waathiriwa wa mafuriko Ethiopia wapelekewa misaada ya dharura na UM

UM wiki hii umeongeza huduma zake za kusafirisha kwa ndege misaada ya chakula na madawa katika eneo la kusini-mashariki ya Ethiopia.

Mshoni wa Zambia kutunikwa zawadi ya UM kwa kupiga vita UKIMWI

Jonsen Habachimba, mshoni kutoka Zambia pamoja na shirika linalojulikana kama Jumuiya ya Maendeleo ya Vijiji ya Mboole (Mboole Rural Development) wametunukiwa zawadi ya dola 20,000, ikiwa ni tunzo la awali la UM kwa mashirika ya kiraia yanayojitolea kushiriki kwenye juhudi muhimu za kupambana na UKIMWI.

Watoto wachanga milioni 1.6 hufa kila mwaka kusini ya Sahara - yaripoti UM

Ripoti ya pamoja kati ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika mengineyo wenzi iliyowasilishwa karibuni kuhusu maendeleo ya afya kwa watoto wachanga imeonya ya kuwa ukanda wa Afrika kusini ya Sahara ndiyo eneo hatari kabisa kuzaa mtoto.~

Huduma za UM kusaidia mamia elfu ya waathiriwa wa mafuriko Kenya

Mashirika ya UM yanayohusika na miradi ya chakula duniani (WFP), wahamiaji (UNHCR), na pia mfuko wa maendeleo ya watoto (UNICEF) yalijumuika nchini Kenya wiki hii kuongoza operesheni za kugawa misaada ya kiutu kwa mamia elfu ya wahamiaji wa Usomali walioajikuta kunaswa na mafuriko yaliozuka kwenye zile kambi walizokuwa wakiishi kaskazini-mashariki ya Kenya.

KM bado anasubiri idhini ya Sudan juu ya vikosi vya mseto vya UM/AU kwa Darfur

KM Kofi Annan alikuwa na mashauriano na Baraza la Usalama wiki hii kuhusu hali katika Darfur,Sudan. Baada ya mkutano wake huo na Baraza la Usalama aliwaambia waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu kwamba Serekali ya Sudan bado haijamtumia jawabu yao ya kuidhinisha maafikiano ya kimsingi, waliokubaliana pamoja wiki iliopita, ya kupeleka vikosi vya mseto vya UM na AU katika Darfur ambayo yanahitajika kidharura kukomesha uhasama na maafa yaliofumka na kutanda kwenye eneo hilo, na kuathiri vibaya maisha ya malaki ya raia.

Mkuu wa OCHA asema LRA inasisitiza kuwepo kuaminiana kufanikiwa kuwasilisha amani Uganda ya kaskazini

Jan Egeland, Makamu Katibu Mkuu juu ya Misaada ya Dharura aliwaarifu wajumbe wa Baraza la Usalama wiki hii kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo karibuni na kiongozi wa waasi wa LRA, Joseph Kony pamoja na maofisa wa Serekali ya Uganda wakati alipozuru bara la Afrika.

Mjumbe wa KM Usomali azikaribisha ahadi za Serekali kushiriki kwenye mazungumzo ya amani

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall amenukuliwa akisema wawakilishi wa wa Serekali ya Mpito ya Usomali waliaahidi kuwa wapo tayari kushiriki tena kwenye yale mazungumzo ya kurudisha amani katika taifa lao kati yao na viongozi wa Kundi la Mahakama za Kiislamu.