Habari Mpya

UNICEF kulaani vitendo vya ubakaji wa watoto Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limelaani vikali sana habari za kutokea vitendo zaidi vya ubakaji huko Zimbabwe na likihimiza sheria mpya kupitishwa kuwalinda watoto wa nchi hiyo na kutoa masomo zaidi juu ya virusi vua HIV na Ukimwi.

Jumuiya ya kimataifa kuisifu Serikali ya JKK

wiki hii jumuiya ya kimataifa imeisifu serekali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa kufanikiwa kutayarisha na kufanya uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur

Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani katika Sudan, UNMIS, limeripoti karibuni ya kuwa wafanyakazi wa kimataifa wanaosimamia huduma za kiutu katika Darfur wanakabiliwa na vizingiti vinavyokwamisha huduma za kuwasaidia raia kupata mahitaji ya kunusuru maisha kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulio na hali ya utumiaji nguvu dhidi yao, pamoja na vitendo vya uharamia na mapigano yalioshtadi kati ya makundi ya waasi.~~

Wanajeshi waangalizi wanne wa UM Kuuwawa Lebanon

Naibu KM wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani Duniani, Jane Holl Lute aliripoti mbele ya Baraza la Usalama wiki hii kwamba wanajeshi waangalizi wanne wa ulinzi wa amani wasiochukua silaha kutoka Austria, Kanada, Finland ~na Uchina, waliuawa Ijumanne kwa mizinga ya majeshi ya Israel ambayo tuliarifiwa ililengwa moja kwa moja, sawia, kwenye kituo cha uangalizi cha UM karibu na mji wa Khiam, Lebanon ya kusini.

UM yaahidi kuongeza misaada ya kiutu Lebanon

Ilivyokuwa matatizo ya kiutu bado yanaendelea kukithiri katika mazingira ya vita katika Lebanon ya kusini UM umeripoti ya kuwa utalazimika kupeleka misafara ziada ya misaada ya kihali katika miji ya Jezzine na Sidon ili kukidhia mahitaji ya kunusuru maisha kwa umma waathiriwa wa maeneo haya. Hatua hii imechukuliwa baada ya msafara wa UM kufanikiwa Ijumanne kupeleka katika mji wa bandari wa Tyre shehena za chakula na mahitaji mengineyo ya kiutu.

Mwakilishi wa KM kwa Usomali apendekeza ujumbe wa kurudisha amani

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall wiki hii amemtumia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kundi la Mahakama za Kiislamu mjini Mogadishu barua inawayohimiza kupeleka wawakilishi wao kwenye duru ya pili ya mazungumzo ya kurudisha amani katika Somalia yaliyoandaliwa kufanyika Khartoum, Sudan kati yao na viongozi wa Serekali ya Mpito ya Usomali.

Kundi la muungano wa waasi (MRC) katika Congo-DRC lasalimisha silaha zao

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kwamba kundi la muungano wa waasi, lijukanalo kwa ufupi kama kundi la MRC, limekubali wiki hii kusalimisha silaha zao.

UNEP yasisitiza umuhimu wa kuboresha hewa Afrika kusini ya Sahara

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) katika mkutano wasiku nne uliofanyika mjini Nairobi, Kenya wiki hii kusailia suala la kuboresha hewa katika miji ya Afrika ametilia mkazo umuhimu wa kubuni ushirikiano mpya ili kukabili tatizo hilo kwa mafanikio.

WFP kufadhiliwa yuro milioni 105 na Kamisheni ya Ulaya

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limepokea msaada wa yuro milioni 105 kutoka Kamisheni ya Ulaya zitakazotumiwa kusaidia huduma za kugawa chakula kwa umma muhitaji wa kimataifa katika 2006.

Katibu Mkuu ahudhuria kikao cha wahisani wa kimataifa kwa Darfur mjini Brussels.

KM Kofi Annan wiki hii alihudhuria kikao maalumu cha wahisani wa kimataifa waliokusanyika katika mji wa Brussels, Ubelgiji kuzingatia uwezekano wa kuchangia msaada maridhawa kufadhilia operesheni za amani za AMIS, yaani vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Afrika (AU) katika Darfur, Sudan.