Habari Mpya

Ban Ki-moon ameapishwa kuwa Katibu Mkuu mpya, na Baraza Kuu kumpongeza Kofi Annan

Alkhamisi tarehe 14 Disemba 2006 Ban Ki-moon kutoka Jamhuri ya Korea, aliapishwa kuwa Katibu Mkuu wa 8 wa UM mbele ya wanadiplomasiya wanaowakilisha Mataifa Wanachama 192 pamoja na wafanyakazi wa Makao Makuu ya UM, katika ukumbi wa Baraza Kuu. Ban aliapishwa na Raisi wa kikao cha 61 cha Baraza Kuu la UM, Sheikha Haya Rashed Al Khalifa wa Bahrain.

Mukhtasari juu ya Mkutano Mkuu wa Pili kuhusu Maziwa Makuu

Mkutano Mkuu wa Pili juu ya Maziwa Makuu ulioandaliwa shirika na UM pamoja Umoja wa Afrika (AU), na kuhudhuriwa na Viongozi sita wa Taifa na Mkuu mmoja wa Serekali, wakiwakilisha mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda na Kenya ulifanyika wiki hii mjini Nairobi.

Baraza Kuu la UM limepitisha Mkataba wa Haki za Watu Walemavu

Mswada wa Mkataba wa Kulinda Haki na Hadhi za Watu Walemavu ulipitishwa, kwa kauli moja, na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kitendo hiki kilikuwa cha historia kuu.

Baraza la Haki za Kiutu kutuma ujumbe wa uchunguzi Darfur

Baraza la UM juu ya Haki za Kiutu wiki hii mjini Geneva limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kupeleka ujumbe maalumu wa watu watano wa hadhi ya juu, katika jimbo la Darfur, Sudan ili kutathminia na kusailia hali ambayo imeripotiwa kufurutu ada katika utekelezaji wa haki za kimsingi kwa raia.

UNHCR yahofia ukiukaji wa haki za wahamiaji wa magendo katika Yemen

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuingiwa na wasiwasi mkuu juu ya ukosefu wa hifadhi kwa wale watu wanaovushwa kimagendo kutoka Afrika kwenye Ghuba ya Aden na majambazi.

ICTR yahukumu kifungo cha miaka 15 kwa aliyekuwa padri Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imepitisha hukumu ya kifungo cha jela cha miaka 15 kwa Athanase Seromba aliyekuwa padri wa Parokia ya Nyange katika kijiji cha Kivumu magharibi ya Rwanda.

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Kitivo cha Haki za Kiutu cha Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini kinachosimamia mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha haki za kimsingi kimetunukiwa zawadi ya dola 10,000 na Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Ripoti juu ya juhudi za karibuni kupiga vita malaria

Hivi karibuni takwimu za UM zilithibitisha ya kuwa watu milioni 300 hadi 500 huambukizwa maradhi ya malaria duniani, kila mwaka, na kati ya idadi hiyo watu milioni 1 hufariki, asilimia kubwa yao ikiwa watoto wachanga kutoka bara la Afrika.

Juhudi za Baraza Kuu kudhibiti biashara haramu ya almasi.

Mnamo mwanzo wa wiki Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio la kuunga mkono Mpango wa Kimberley na kupendekeza utaratibu huo uendelea kuimarishwa kimataifa. Kabla ya azimio kupitishwa Mataifa Wanachama 192 wa UM walisikia ripoti ya mapitio kutoka Raisi Festus Gontebanye Mogae wa Botswana, Mwenyekiti wa mwaka huu wa nchi zilizoridhia na kuidhinisha Mpango wa Kimberley.

Vurugu la Darfur huenda likaathiri mataifa jirani aashiria KM

KM wa UM ameelezea kuchukizwa sana kwa kufumka tena, hivi karibuni, katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur, vurugu na wasiwasi. Hali hiyo ilisababisha idadi kubwa ya raia wa Darfur kuhajiri maskani yao ili kunusurisha maisha.