Habari Mpya

Watoto wachanga milioni 1.6 hufa kila mwaka kusini ya Sahara - yaripoti UM

Ripoti ya pamoja kati ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika mengineyo wenzi iliyowasilishwa karibuni kuhusu maendeleo ya afya kwa watoto wachanga imeonya ya kuwa ukanda wa Afrika kusini ya Sahara ndiyo eneo hatari kabisa kuzaa mtoto.~

Huduma za UM kusaidia mamia elfu ya waathiriwa wa mafuriko Kenya

Mashirika ya UM yanayohusika na miradi ya chakula duniani (WFP), wahamiaji (UNHCR), na pia mfuko wa maendeleo ya watoto (UNICEF) yalijumuika nchini Kenya wiki hii kuongoza operesheni za kugawa misaada ya kiutu kwa mamia elfu ya wahamiaji wa Usomali walioajikuta kunaswa na mafuriko yaliozuka kwenye zile kambi walizokuwa wakiishi kaskazini-mashariki ya Kenya.

KM bado anasubiri idhini ya Sudan juu ya vikosi vya mseto vya UM/AU kwa Darfur

KM Kofi Annan alikuwa na mashauriano na Baraza la Usalama wiki hii kuhusu hali katika Darfur,Sudan. Baada ya mkutano wake huo na Baraza la Usalama aliwaambia waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu kwamba Serekali ya Sudan bado haijamtumia jawabu yao ya kuidhinisha maafikiano ya kimsingi, waliokubaliana pamoja wiki iliopita, ya kupeleka vikosi vya mseto vya UM na AU katika Darfur ambayo yanahitajika kidharura kukomesha uhasama na maafa yaliofumka na kutanda kwenye eneo hilo, na kuathiri vibaya maisha ya malaki ya raia.

Mkuu wa OCHA asema LRA inasisitiza kuwepo kuaminiana kufanikiwa kuwasilisha amani Uganda ya kaskazini

Jan Egeland, Makamu Katibu Mkuu juu ya Misaada ya Dharura aliwaarifu wajumbe wa Baraza la Usalama wiki hii kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo karibuni na kiongozi wa waasi wa LRA, Joseph Kony pamoja na maofisa wa Serekali ya Uganda wakati alipozuru bara la Afrika.

Mjumbe wa KM Usomali azikaribisha ahadi za Serekali kushiriki kwenye mazungumzo ya amani

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall amenukuliwa akisema wawakilishi wa wa Serekali ya Mpito ya Usomali waliaahidi kuwa wapo tayari kushiriki tena kwenye yale mazungumzo ya kurudisha amani katika taifa lao kati yao na viongozi wa Kundi la Mahakama za Kiislamu.

Wavusha magendo walisafirisha halaiki ya Wasomali kwenye Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba katika mwaka huu pekee Wasomali 22,000 walihatarisha maisha walipojaribu kuvuka Ghuba ya Aden, kutokea Usomali na kuelekea Yemen, kwa kutumia mashua zilizoregarega na zisiokuwa imara.

Kenya kuchachamaa kutunza mazingira dhidi ya uharibifu wa hali ya hewa

KM wa UM Kofi Annan alipohutubia kikao cha wawakilishi wa Hadhi ya Juu kwenye Mkutano Mkuu juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa alisisitiza ya kuwa ni lengo la jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwepo maelewano mazuri miongoni ya watu, na vile vile kuhakikisha kuna mlingano wa kimaumbile kati ya wanadamu na mazingira asilia, mazingira ambayo uhai wetu huyategemea kumudu maisha.

Mapitio ya Mkutano wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Ulimwenguni

Kuhusu ripoti nyengine zinazoambatana za Mkutano wa Nairobi, Yvo de Boer, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya UM ya Mfumo wa Mkataba juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Ulimwenguni (UNFCCC) alinakiliwa akisema aliridhika na mafanikio yaliopatikana kwenye Mkutano wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Ulimwenguni.

Mapigano ya kikabila nchini Chad yasababisha vifo 200

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kufumka kwa mapigano ya kikabila hivi majuzi katika mashariki-kusini ya Chad.

Wagombea uraisi DRC wanasihiwa na KM kujiepusha na lugha ya uchochezi baada ya matokeo kutangazwa

Katibu Mkuu (KM) amewasihi Raisi Joseph Kabila, Makamu Raisi Jean-Pierre Bemba na wafuasi wao kuridhia, kwa pamoja, na bila ya fujo matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo)