Habari Mpya

Mamilioni ya watu zaidi wahitaji msaada wa chakula Ethiopia kutokana na machafuko Kaskazini mwa nchi:WFP

Idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula kaskazini mwa Ethiopia imeongezeka na kufikia takriban watu milioni 9.4 na hii ni kutokana na vita inayoendelea nchini  humo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. 

Kenya tuna mengi ya kujivunia na expo2020 ni fursa ya kuyaonesha:Macheso

Maonesho ya kimataifa au Expo2020 ambayo mwaka huu yanafanyika Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu au Emarati ni fursa nzuri ya washiriki kutoka kila pembe ya dunia kunadi uwezo wao katika Nyanja mbalimbali iwe kilimo, biasahara, nishati, teknolojia na kadhalika lengo likiwa kuvutia fursa za kibiashara, ushirikiano, utalii  na hata uwekezaji.

Msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia waleta raha baada ya karaha

Mizozo, majanga ya kibinadamu na ongezeko la majanga yatokanayo na tabianchi yamesababisha viwango vya juu vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, hali ambayo imshika kasi zaidi wakati wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19. Kitendo hicho kimechangia udharura wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.
 

Kutozingatia masharti ya matumizi ya viuavijiumbe maradhi ndio chachu ya usugu wa dawa:FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema ongezeko la usugu wa viuavijiumbe maradhi yaani dawa zinazopambana na vimelea vya maradhi unatokana kwa kiasi kikubwa na kutozingatia marshi ya matumizi ya dawa hizo hususani katika kilimo na ufugaji. 

COVID-19 yachochea madhila ya ukatili dhidi ya wanawake :UN WOMEN

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa UN Women iliyoangazia athari za janga la COVID-19 kwa usalama wa wanawake nyumbani na katika maeneo ya umma imeonesha kuwa hisia za usalama za wanawake zimepotea, na kusababisha athari mbaya kwa hali yao ya kiakili na kimihemko.

Akiwa Colombia, Guterres ajionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Colombia, amejionea maendeleo na changamoto za mkataba wa amani uliofikiwa nchini humo miaka mitano iliyopita kati ya serikali na wapiganaji wa zamani wa kikundi cha FARC.

WHO yatangaza leseni ya wazi ya utafiti wa kupamba na COVID-19

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na lile la hati miliki za dawa MPP hii leo wametangaza leseni ya kwanza ya uwazi ya kimataifa ya teknolojia inayohusiana na COVID-19 iliyotolewa na baraza la kitaifa la utafiti la Hispania CSIC.

Yemen njaa na magonjwa vinakatili maisha ya watu wengi kuliko vita:UNDP

Vifo vingi nchini Yemen vinatokea kutokana na athari za mzozo kwa bei ya vyakula na kuzorota kwa hali ya usafi.  

Mifumo ya uzalishaji na usambazaji wa mazao ya chakula iimarishwe- FAO

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya chakula na kilimo duniani SOFA2021, imezitaka nchi duniani kuhakikisha mifumo yao ya kilimo cha mazao ya chakula ina uwezo wa kuhimili changamoto zozote zinazoweza kutokea kama vile janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19, ambalo limesababisha ongezeko la njaa duniani.
 

Miaka mitano baada ya makubaliano ya amani, Llano Grande Colombia waunda familia kutoka sehemu tofauti.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaelekea Colombia wiki hii kuadhimisha miaka mitano tangu kutiwa saini kwa mapatano ya amani yaliyomaliza miaka 50 ya mzozo nchini humo, na shughuli zake zitajumuisha kusafiri hadi katika kijiji cha Llano Grande, ambako wakazi wa mji huo. na wapiganaji wa zamani wanafanya kazi pamoja ili kupata maisha bora ya baadaye.