Habari Mpya

Mshauri Maalumu wa KM akutana na Raisi wa Rwanda

Juan Mendez, Mshauri Maalumu wa KM wa Kuzuia Mauaji ya Halaiki majuzi amezuru Rwanda na alikutana kwa majadiliano na Raisi Paul Kagame.

Baazala Usalama kuongeza mudawa operesheni za mashirika matatu ya ulinzi wa amani Afrika

Baraza la Usalama limepitisha maazimio ya kuongeza muda wa kazi za yale mashirika ya UM juu ya ulinzi wa amani katika Ethiopia na Eritrea (UNMEE), na katika JKK (MONUC) na pia katika Liberia (UNMIL).

Kamati ya Utendaji ya UNHCR yakutana mjini Geneva

Antonio Gutteres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Wahamiaji la UNHCR, alipofungua rasmi, wiki hii, mijadala ya Kamati ya Utendaji mjini Geneva alishauri ya kwamba “wakati wa kuambizana ukweli” umewadia.

Uchaguzi wa KM mpya wa Umoja wa Mataifa unanyemelea

Ijumatatu tarehe 09 Oktoba (2006) Baraza la Usalama linatazamiwa kupiga kura ya kumteua rasmi KM mpya atakayechukua nafasi ya KM Kofi Annana mnamo mwanzo wa 2007. Baada ya hapo Baraza la Usalama litatuma jina la KM mpya mbele ya Baraza Kuu kuidhinishwa na wawakilishi wa kimataifa.

Tabaka la hewa kingifu la ozone katika Antartica limeharibiwa kima kikubwa katika 2006

Shirika la UM juu ya Vipimo vya Hali ya Hewa (WMO) limeripoti ya kwamba tabaka la hewa kingifu la ozone katika eneo la ncha ya kusini ya dunia la Antartica, limethibitika kuharibiwa kwa kima kikubwa kabisa mno mwaka huu. Uharibifu huu husababisha miale ya jua kupenya kwa wingi zaidi kwenye mazingira ya kimataifa, na hukithirisha maradhi ya sartani kwa umma wa ulimwengu.

WHO yahimiza huduma za usafi wa hewa katika miji

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza serekali zote za kimataifa kuongeza huduma zao katika kuboresha usafi wa hewa katika miji yao. WHO ilisema pindi hatua hii itachukuliwa na miji husika itasaidia kuhifadhi afya na maisha ya watu milioni 2 ambao hufariki kila mwaka duniani kutokana na uharibifu wa hewa.~~

Juhudi za kupunguza umasikini katika nchi zenye uchumi mdogo (Sehemu ya Pili)

Hivi karibuni wajumbe wa kimataifa walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM, mjini New York, kuhudhuria Mkutano Mkuu maalumu wa Baraza Kuu, uliofanya mapitio juu ya utekelezaji wa ule Mpango wa Utendaji wa Brussels wa 2001. Mkutano huo wa Daraja ya Juu ulisailia juhudi za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika yale mataifa 50 yenye uchumi wa kima cha chini kabisa, mataifa ambayo hujulikana kama LDCs.~~

Maelfu ya wahamiaji wa Usomali wakimbilia Kenya kunusuru maisha

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti ya kuwa maelfu ya wahamiaji kutoka Usomali wanakimbilia Kenya hivi sasa kukwepa mapigano yaliofumka karibuni nchini mwao baina ya wafuasi wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) na vikosi vya Serekali ya Mpito.

UNICEF yawakilisha ripoti kuhusu maamirisho ya lengo la MDGs juu ya maji safi na usafi wa mastakimu

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Ann Veneman Alkhamisi aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa, ripoti yenye kuelezea maendeleo yaliopatikana kuhusu utekelezaji wa lengo la MDGs la kuimarisha huduma za maji safi na usafi wa mastakimu. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF, tangu 1990 watu bilioni 1.2 walifanikiwa uwezo wa kupata maji ya kunywa safi na salama.

Mjadala wa wawakilishi wote kuhitimishwa kwenye Baraza Kuu la UM

Mjadala wa wiki mbili wa wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu la UM ulihitimishwa hapo Ijumatano kwa moyo mzito. Mjadala huu, wa kikao cha 61 cha Baraza Kuu, ulihudhuriwa na maofisa mbalimbali, wa vyeo vya juu, kutoka Serekali wanachama, maofisa ambao wingi wao walihimizana kuongezwe uangalifu wa jumla miongoni Mataifa Wanachama, ili kuhifadhi heshima na hadhi ya UM katika kazi zake.