Ripoti mpya kuhusu hali ya ukimwi duniani imetoa matumaini baada ya kubainika kuwa asilimia 75 ya watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi, VVU wanatambua hali zao.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa María Fernanda Espinosa, amesema anaelewa fika uamuzi wa baadhi ya mataifa wa kutokuwa tayari kutia saini makubaliano mapya kuhusu uhamiaji baadaye mwaka huu.
Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni janga la kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia tukio maalum la siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake lililofanyika kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani hii leo.
Kila siku ajali za barabarani hukatili uhai wa maelfu ya watu, kuwaacha wengine na ulemavu wa maisha na kuathiri mustakhbali wa familia nyingi duniani. Na wakati wa kuchukua hatua dhidi ya zahma hiyo ni sasa limesema shirika la afya duniani, WHO.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Mohamed Ahmed Eldirdiri amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa mazingira ya sasa yanatia moyo katika kupatia suluhu masuala yote yaliyosalia kati ya nchi yake na Sudan Kusini.
Taka zilizokithiri katika makazi ya binadamu ni lazima zidhibitiwe la sivyo zitaweka hatarini sio tu mazingira bali afya zao. Wito huo umetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT hii leo katika kuadhimisha siku ya makazi duniani.
Naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Muallem amesema vita vya nchi yake dhidi ya ugaidi vinaelekea ukingoni akishukuru ujasiri, dhamira, umoja wa watu wa Syria, jeshi la nchi hiyo, msaada wa marafiki na washirika wao.