Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza mwelekeo wake mpya kuhusu udhibiti wa silaha katika juhudi za kutokomeza silaha za nyuklia pamoja na silaha zingine zinazoweza kusababisha maangamizi dunia kutokana na makosa iwe ya kiufundi, kielektroniki au ya kibinadamu.
Hii leo WHO ilikuwa na kikao cha kamati ya dharura kuangazia iwapo mlipuko wa Ebola huko DRC unasababisha udharura katika afya ya umma ulimwenguni au la. Wataalamu wamekutana na kumshauri Mkurugenzi Mkuu naye ametangaza uamuzi wake.