Habari Mpya

UM inahitajia kufadhiliwa msaada ziada wa kijeshi kwa Darfur

Idara ya UM juu ya Operesheni za Ulinzi wa Amani Duniani (DPKO) imeripoti kutofanikiwa kufadhiliwa na nchi wanachama misaada ya vifaa na zana nzito nzito za kijeshi, pamoja na helikopta, vifaa ambavyo vinahitajika kutumiwa na vikosi mseto vya Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa, vitakavyojulikana kama vikosi vya UNAMID, vitakavyopelekwa Darfur, Sudan mwisho wa mwaka.

Operesheni za UNMIL kuongezewa muda kukuza amani Liberia

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuendeleza operesheni za shirika la UM la ulinzi wa amani katika Liberia (UNMIL) kwa miezi 12 ziada hadi Septemba 30 2008.

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya Ulimwenguni (UNDOC), ikijumuika na Benki Kuu ya Dunia, wameanzisha Taratibu za kisheria Kuhakikisha Mali za Umma Zilioibiwa Zinafidiwa, kitendo kilichokusudiwa kuyasaidia mataifa masikini kurejeshewa rasilmali ya taifa iliyoibiwa na viongozi walaji rushwa, ambao walizipatia akiba hizo hifadhi kwenye vyombo vya fedha vya kigeni; fedha hizi zitakapopatikana zinatarajiwa kutumiwa kuendeleza huduma za kiuchumi na jamii zenya natija kwa taifa zima.~

Vijana wa kimatifa wakutana Ujerumani kusailia udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni

Hivi majuzi wajumbe vijana 180 ziada kutoka mataifa 85 wanachama walikusanyika katika mji wa Leverkusen, Ujerumani kuhudhuria mkutano mkuu uliokuwa na makusudio ya kusailia taratibu za kuendeleza teknolojiya ya kisasa katika huduma za kuhifadhi mazingira katka ulimwengu. Asilimia kubwa ya vijana hawa walitaka kuhakikisha vizazi vya siku zijazo, hawatoelemewa tena na mzigo wa kimaisha unaotokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani. ~~Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.~~Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Juhudi za Kimataifa za kupiga marufuku mila ya kukeketwa wasichana kote duniani

Watalamu kutoka sehemu mbali mbali za dunia pamoja na wajumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya kiserekali, maafisa wa idara za usalama na wa serekali, walikutana mjini Addis Abeba mapama mwezi wa Agosti kutathmini na kujadili njia za kukomesha kabisa mila ya kukeketa wasichana.

Utumizi wa musiki katika kuhamasisha watu juu ya masuala ya kijamii

Mwaka 1954 Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF lilianza kuomba msaada wa watu mashuhuri hasa wasani, waimbaji na wachezaji michezo tofauti kutumia uwezo na umashuhuri wao kuhamasisha watu juu ya haki za watoto na masuala mengine yanayo husiana na watoto. Mtu wa kwanza alikua Danny Kaye aliyekua mtumbuizaji na msani mashuhiri sana aliyefariki 1987 akiwa balozi wa nia njema wa UNICEF.

Uchina itajitahidi kujihusisha kikamilifu kuleta suluhu maridhia Darfur

Mjumbe wa Uchina juu ya Suala la Darfur, Balozi Liu Guijin alizuru Makao Makuu mwanzo wa wiki na alikutana na wawakilishi wa jamii ya kimataifa pamoja na KM Ban Ki-moon. Kadhalika alichukua fursa hii na kufanya mazungumzo na Idhaa ya Redio ya UM ambapo alihojiwa na Fan Xiao wa vipindi vya Kichina. Balozi Liu aliombwa aelezee sababu hasa zilizoifanya Serekali ya Uchina kuamua kuteua Mjumbe Maalumu kushughulikia suala la Darfur?:

Katibu Mkuu ameitisha mkutano wa aina ya pekee kuimarisha maendeleo Afrika

Ripoti ya mwezi Juni (2007) ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) ilibainisha mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara bado yamepwelewa sana kwenye juhudi za maendeleo, kwa ujumla, na hakuna dalili haya yatafanikiwa kuyakamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ya kupunguza kwa nusu, kabla ya 2015, umasikini, njaa, maradhi na kutojua kusoma na kuandika.

Baraza Kuu lapitisha Mwito wa Kihistoria juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Alkhamisi Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kihistoria lililoelezea haki za kimsingi kwa watu milioni 370 duniani wenye kutambuliwa kama ni wenyeji wa asili. Azimio limeharamisha ubaguzi wote dhidi ya fungu hili la kimataifa ambalo lilikuwa likitengwa kimaendeleo na nchi zao kwa muda mrefu.

WHO inajitahidi kudhibiti homa ya Ebola katika DRC ya kati

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii limepeleka misaada ya afya ya dharura katika jimbo la mashariki la Kasai Occidental, DRC baada ya kufumka kwa homa maututi ya Ebola katika wiki za karibuni.