Habari Mpya

Juhudi za kuimarisha uzazi salama huko Tanzania

White ribbon alliance ni mungano wa kimataifa wa watu na mashirika uloundwa kuhamasisha wananchi juu ya haja ya kuwepo na afya nzuri na usalama kwa wanawake wote wajazito na wanapojifungua pamoja na watoto wanaozaliwa.

Mzozo wa Darfur unavyosababisha matatizo ya usalama kwa majirani wa Sudan.

Wakati majadiliano yanaendelea kwenye baraza la usalama katika kumaliza kuandika azimio litakalo ruhusu kupelekwa kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Jumuia ya afrika huko Darfur, mzozo huo katika eneo la magharibi ya Sudan umekua na athari kubwa kwa majirani zake Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

UM yatoa mwito kwa pande zote Sierra Leone kuepusha ghasia kabla uchaguzi.

UM umetoa mwito kwa vyama vyote vya kisiasa huko Sierra Leone kujiepusha kutumia matusi na maneno ya uchochezi yanayoweza kusababisha ghasia kabla ya uchaguzi wa rais na wa bunge wa mwezi ujao. Mwakilishi maalum wa katibu mkuu Victor Angelo akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mkutano wa kitaifa juu ya majadiliano na vijana alisema, inabidi tufahamu matukiyo ya hivi karibuni ya ghasia za kisiaasa.

Msaada wa kwanza wa Zambia kwa WFP unasaidia kupunguza upungufu wa chakula.

Program ya Chakula Duniani WFP, imepongeza mchango wa kwanza kabisa kutoka kwa serekali ya Zambia, ambao utawawezesha maelfu ya wa Zambia kupokea msaada muhimu wa chakula baada ya Septemba.

UM kusaidia polisi wa Liberia kufikia viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Mjumbe maalum wa UM huko Liberia amekabidhi kwa Kikosi cha Polisi cha Taifa, jengo lililo karabatiwa upya la kuwaweka wafungu kulingana na masharti muhimu kabisa ya viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Mkuu wa huduma za dharura wa UM yuamulika atahri za ukame huko Kusini mwa Afrika.

Mratibu wa huduma za dharura wa UM, Bw John Holmes alimulika wiki hii atahri za ukame sugu unaokumba nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika, akisisitiza kwamba hali ni mbaya zaidi huko Swaziland. Alisema wanatarajia matatizo makubwa ya ukosefu wa akiba ya chakula katika eneo hilo.

Ethopia: mkuu wa haki za binadam wa UM apongeza kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.

Kamishna mkuu wa haki za binadam wa UM amekaribisha msamaha na kuachiliwa hivi karibuni zaidi ya viongozi wa kisiasa na wakereketwa 30 huko Ethopia na kuhimiza kuwepo na utaratibu wa haki kwa madarzeni ya washtakiwa ambao baado kesi zao hazi kumalizika.

Mkutano juu ya mzozo wa Darfur unmepangwa kufanyika mapema Augusti.

Wajumbe maalum wa UM na AU wakiendelea na juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa kwa ajili ya ugomvi wa jimbo la Darfur huko Sudan, wamewaalika viongozi wa makundi ambayo hayakutia sahihi makubaliano ya amani kwa mazungumzo ya ‘majadiliano ya awali’ yaliyopangwa kuanza mapema mwezi ujao huko Arusha Tanzania.

Kwa habari za hapa na pale

Mashirika ya huduma za dharura ya UM yanapeleka kwa haraka misaada ya chakula na afya kusini mwa Sudan ambako mvua kali mnamo siku za hivi karibuni zimesababisha mafuriko yaliyowathiri karibu watu elfu 10. Shirika la watoto la UM, UNICEF limeshapeleka mikoba midogo 1 500 madawa na vitu vya dharura, pamoja na chakula cha siku 15.

Zowezi la kuwapokonya silaha wapiganaji katika DRC

Awamu ya tatu ya kuwapokonya silaha, na kuwarudisha katika maisha ya kiraia au kujiunga na jeshi la taifa, kwa ajili ya makundi matatu ya waasi huko Ituri, ilianza mapema mwezi wa Julai.