Habari Mpya

Fafanuzi za kikao cha mwaka cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Umma wa kimataifa unaotambuliwa rasmi na UM kama ni jamii ya wenyeji wa asili, karibuni walikamilisha hapa Makao Makuu kikao cha mwaka cha wiki mbili.

Naibu KM aonya "Afrika imepwelewa kutekeleza MDGs"

Naibu KM Asha-Rose Migiro aliwasilisha ripoti mpya ya UM kuhusu maendeleo katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)katika mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara. Alionya ya kuwa juhudi za kuyakamilisha malengo hayo kwa wakati ziko nyuma na zinazorota.

Jamii ya kimataifa yaadhimisha 'Siku ya Mazingira Duniani'

Tarehe 05 Juni huadhimishwa kila mwaka kuwa ni \'Siku ya Mazingira Duniani\'. Sherehe aina kwa aina hufanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yaliopo New York na katika sehemu nyengine za ulimwengu ambapo UM huendeleza shughuli zake.~

Juhudi za kufufua amani katika Darfur

Jan Eliasson, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Darfur alikuwa na mashauriano ya faragha na Baraza la Usalama kuhusu juhudi za kufufua huduma za usalama na ulinzi wa amani katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Afrika kutawala ajenda ya Baraza la Usalama mwezi Juni

Balozi Johan C. Verbeke wa Ubelgiji, ambaye taifa lake limeshika madaraka ya uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, aliwaambia waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu kuwa kwamba anaashiria kuwepo “ajenda nzito” katika mijadala ya mwezi huu ya Baraza, na wingi wa mada zitakazozingatiwa kwenye Baraza, alisisitiza, zitahusu masuala ya Afrika.

Usomali kufadhiliwa msaada wa kihali na UM

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Misaada ya Dharura ya Kiutu (CERF) inatarajiwa kuifadhilia Usomali msaada wa dola miloni 3 ambazo zitatumiwa kupeleka kwenye yale maeneo ya Mogadishu yalioathirika na mapigano, kwa kutumia usafiri wa ndege, wafanyakazi wa mashirika yasio ya kiserekali na kupeleka misaada ya kihali kwa umma muhitaji. Kwa mujibu wa taarifa za UM eneo la Usomali sasa linakabiliwa na tatizo la mvua, hali ambayo huzorotisha huduma za usafiri wa kwenye barabara.

Hali ya chakula katika Zimbabwe inaregarega; UNICEF kusaidia kuchanja watoto dhidi ya polio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) pamoja na mashirika wenzi yameanzisha kampeni ya pamoja ya kuwapatia watoto milioni 2 nchini chanjo dhidi ya maradhi ya kupooza (polio) katika Zimbabwe, hasa ilivyokuwa asilimia kubwa ya raia inakabiliwa na matatizo yanayosababishwa na kuporomoka kwa maendeleo ya uchumi kitaifa.

Kesi ya Charles Taylor kuanzishwa mjini Hague

KM Ban amepongeza kuanzishwa kwa kesi ya aliyekuwa Raisi wa Liberia, Charles Taylor katika mji wa Hague, Uholanzi na Mahakama Maalumu ya Sierra Leone dhidi ya Jinai ya Vita. Taylor alituhumiwa kuongoza vitendo karaha viliokiuka sheria na kupalilia uhasama miongoni mwa vikundi vya kizalendo vilivyokuwa vimeshiriki kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Sierra Leone.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amepokea kwa moyo thabiti maafikiano yaliofikiwa na viongozi wa kundi la G-8 kwenye mji wa Heiligendamm, Ujerumani ambapo walikubaliana kuchukua hatua za mapema, na zenye nguvu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, na kuahidi kutumia mfumo wa Umoja wa Mataifa (UM) katika kuitekeleza miradi hiyo.

Tatizo la athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye miji

Ripoti ya Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) imeashiria ya kuwa katika mwaka 2007 tutashuhudia mabadiliko hakika kwenye tabia ya wanadamu, kwa ujumla, ambapo inaripotiwa fungu kubwa la umma wa kimataifa, utahajiri na kuukwepa utamaduni wa vijijini, kitendo ambacho kitawapatia umma huu utambulisho mpya na kujulikana kama viumbe vya miji, au kwa lugha ya KiLatina homo urbanus.