Habari Mpya

Juhudi za UM kudhibiti maradhi ya vijidudu vinavyodhuru ngano

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kugundua aina ya vijidudu vijiyoga vipya, vyenye uwezo wa kuzusha maambukizo haribifu makubwa ya mazao ya ngano, vijidudu ambavyo vimeshuhudiwa kusambaa kwenye maeneo yalioanzia Afrika Mashariki - ikijumuisha mataifa ya Ethiopia, Kenya na Uganda – na kuenea hadi Yemen, kwenye Ghuba ya Bara Arabu.

Jumuiya ya kimataifa yasikitika na kulaani mashambulio ya mabomu Algeria na Iraq

Maofisa wa UM wa vyeo vya juu, wakijumuika na KM Ban Ki-moon walishtumu na kulaani vikali mashambulio maututi yaliotukia majuzi kwenye Bunge la Iraq, Baghdad, ambapo Wabunge kadha walifariki na wingi wengineo kujeruhiwa.

Maendeleo Sudan kusini kuleta marekibisho kwenye operesheni za WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa itaanza kupunguza polepole operesheni za kuhudumia misaada ya dharura Sudan ya kusini, na badala yake kuanzisha miradi mipya ya muda mrefu ya kufufua kilimo, kwa sababu viashirio vimethibitisha mahitaji ya misaada ya kihali mwaka huu yatateremka kwa khumsi moja.

Hali mbaya kusini-mashariki ya Chad imekiuka makadirio ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imeripoti ya kuwa hali kusini-mashariki ya Chad imeharibika sana na imekiuka makadirio, mazingira ambayo yalijiri baada ya kufanyika mashambulio ya kikatili, na makundi yenye silaha, dhidi ya wanavijiji, mnamo mwisho wa mwezi Machi.

Mapigano makali Usomali kuzusha msiba mkuu wa kiutu nchini: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali ya kijamii, kwa ujumla, katika Usomali, ni mbaya sana kwa sasa, kutokana na mapigano makali yalioshtadi karibuni, vurugu ambalo aina yake haijawahi kushuhudiwa tangu 1991.

Meli iliokodiwa na WFP na kutekwa nyara Usomali imeachiwa huru

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limepongeza kuachiwa huru kwa ile meli ya MV Rozen, ambayo iliikodi siku za nyuma kupeleka chakula Usomali. Meli hiyo ilitekwa nyara na maharamia kwenye mwambao wa eneo la Puntland mnamo Februari 25 mwaka huu.

MONUC ilimsaidia kiongozi wa upinzani DRC kupata kibali cha kwenda Ulaya kwa matibabu

Ripoti za UM zimethibitisha kuwa Shirika linalohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) lilishiriki kwenye mazungumzo na wenye madaraka nchini DRC ya kumpatia Seneta Jean-Pierre Bemba ruhusa ya kufanya safari ya kwenda Ulaya kwa matibabu.

Tume ya wataalamu wa UM kwenda Bukini kuratibu mradi wa kuwasaidia waathiriwa wa vimbunga

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetuma Bukini timu maalumu ya wataalamu watano watakaofanya uchunguzi wa mahitaji ya kihali katika eneo hilo, na pia kuandaa utaratibu wa kuhudumia misaada ya kimataifa kwa umma ulioathirika na maafa ya vimbunga, maafa asilia ambayo yalileta uharibifu mkubwa kwenye taifa hilo la kisiwa.

Hapa na pale

WHO imepongeza uamuzi wa karibuni wa kampuni ya madawa ya Maabara ya Abbott (Abbott Laboratories) wenye dhamira ya kupunguza bei ya zile dawa za kurefusha maisha zinazojulikana kama LPV/R, ambazo huuzwa kwenye soko la kimataifa kwa kutumia jina la Kaletra/Aluvia, na hupewa wagonjwa wenye VVU na UKIMWI.~

Uchambuzi wa Mjumbe wa Kenya juu ya kikao cha 51 cha CSW

Kamisheni ya UM juu ya Haki za Wanawake (CSW)ilikamilisha kikao cha mwaka cha wiki mbili hivi karibuni ambapo maelfu ya wajumbe wa kiserekali na mashirika ya kiraia walijumuika kuzungumzia taratibu za kuchukuliwa kipamoja, ili kuharakisha utekelezaji wa maazimio na mikataba iliopitishwa siku za nyuma iliokuwa na makusudio ya kuliziba pengo la tofauti za kijinsia.