Habari Mpya

Watoto milioni 4.5 Ghana watapatiwa matibabu dhidi ya minyoo

Wiki ijayo UNICEF, ikishirikiana na idara za ilimu na afya katika Ghana wanatarajiwa kujumuika kuanzisha huduma za siku nne zenye dhamira ya kuwapatia watoto milioni 4.5 waliopo katika skuli za serekali 28,000, matibabu dhidi ya maradhi ya minyoo.

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Pili)

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Michele Montas hivi majuzi alizuru mtaa wa mabanda wa Mathare katika vitongoji vya Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Kwanza)

Hivi karibuni, aliyekuwa mwandishi habari wa Idhaa ya Redio ya UM, Michele Montas alizuru Kenya kuangalia namna mashirika wenzi na UM yanavyoendeleza huduma za kupunguza umasikini, hasa miongoni mwa ule umma wenye kuishi kwenye mazingira ya hali duni.

Kesi ya Charles Taylor kuanza mwanzo wa Juni mjini Hague

Stephen Rapp, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama Maalumu ya Sierra Leone juu ya Jinai ya Vita aliarifu wiki hii kuwa kesi ya aliyekuwa Raisi wa Liberia, Charles Taylor, inatazamiwa kuanza katika mji wa Hague, Uholanzi tarehe 04 Juni 2007. Taylor alifunguliwa mashitaka yenye kumtuhumu kuhusika na vitendo vilivyokiuka haki za kimsingi dhidi ya raia wa Sierra Leone wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe viliposhtadi.

Umma ulion'golewa mastakimu Usomali kupatiwa makazi mapya

Mashirika sita ya UM, yakijumuika na Shirika lisio la kiserekali la kutoka Uholanzi lijulikanlo kama Baraza la Huduma za Wahamiaji la Kidachi,pamoja na jumuiya za kienyeji ziliopo katika mji wa bandari wa Bosaso, Usomali ya kaskazini wamejumuika kuhudumia mpango maalumu wa majaribio wenye lengo la kuzipatia aila 120 zilizong’olewa makwao baada ya mapigano kufumka, makazi mapya. Vile vile familia 30 nyengine masikini kutoka eneo la Bosaso nazo zitafadhiliwa makazi.

WFP yashtumu mashambulio dhidi ya misfara yake nchini Chad

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeshtumu vikali utekaji nyara na mashambulio yaliyofanyika mwisho wa wiki iliopita, dhidi ya misafara ya magari matupu 48 yaliokuwa yakirejea katika mji wa Khufra, Libya ya kusini kutokea Chad ya Mashariki. Haya ni mashambulio ya tatu dhidi ya misafara ya WFP katika miezi miwili iliopita.