Habari Mpya

Walinda amani watatu wa MINUSCA kutoka Tanzania wamejeruhiwa nchini CAR 

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzaina wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ujulikanao kama  MINUSCA wamejeruhiwa jana Alhamisi katika kijiji cha Batouri Bole, mkoani Mambéré-Kadéï baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi. 

WFP imesitisha opereshen El Fasher Sudan kufuatia mashambulizi katika maghala yake

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limelazimika kusitisha operesheni zake kwenye jimbo zima la Darfur Kaskazini kufuatia mfululizo wa mashambulizi katoika maghala yake yote matatu kwenye mji mkuu wa jimbo hilo El Fasher. 

Ukiukwaji wa haki za mtoto duniani umeshamiri- UNICEF

Mwaka 2021 ukifikia ukingoni hii leo, shirika la Umoja wa Matafa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za Watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya.

Mwaka 2022 uwe mwaka wa kutokomeza janga la Corona na kuimarisha sekta ya afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesema bado lina matumaini kuwa mwaka 2022 unaweza kuwa mwaka sio tu wa kutokomeza awamu mbaya ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 bali pia kusaka mbinu thabiti za kuwa salama zaidi kiafya.
 

Chonde chonde , tunawanusru wakimbizi wa Rohingya waliokwama ndani ya boti Aceh:UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito wa kuruhusiwa haraka iwezekanavyo kutia nanga kwa boti iliyosheheni wakimbizi wa Rohingya huko pwani ya Bireuen jimboni Aceh nchini Indonesia, boti ambayo yaelezwa haina viwango na inaweza kuzama wakati wowote huku abiria wengi wakiwa ni wanawake na watoto.  

UNHCR yaomboleza kifo cha mfanyakazi wake aliyeuawa Ethiopia 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na kifo cha mfanyakazi mwenzao kilichotokea Kaskazini mwa Ethiopia kutokana na machafuko yanayoendelea. 

Wakimbizi Hoima, Uganda, waishukuru UN kwa ulinzi mwaka 2021

Kuelekea mwaka mpya wa 2022 wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali wilaya ya Hoima nchini Uganda wametoa shukrani zao kwa Umoja wa Mataifa huku wakiomba usaidizi zaidi mwaka ujao wakati huu ambapo bado kuna changamoto za kimaisha zinazosababishwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
 

Watu 31 wafa maji wakiwa safarini kuingia barani Ulaya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesikitishwa na vifo vya hivi karibuni vya watu 31 waliokufa maji katika matukio matatu tofauti ya kuzama kwa boti kwenye bahari ya Aegean.

Operesheni ya MINUSCA yawafurusha wapiganaji wa UPC mjini Boyo, CAR 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, tarehe 25 Desemba mwaka huu umeanzisha operesheni ya kuwatimua wanakundi takribani 200 wa kundi linalojihami kwa silaha la Unity for Peace in Central Africa, UPC kutoka mji wa Boyo, mkoani Ouaka. 

Ni muhimu makubaliano ambayo ni msingi wa uchaguzi yatekelezwe Somalia – Wadau wa kimataifa 

Taarifa iliyotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM hii leo mjini Mogadishu, Somalia imeeleza kwamba wadau wa kimataifa wanafuatilia kwa wasiwasi mkubwa hali ya sasa na maendeleo ya kisiasa nchini Somalia.