Baada ya karibu miaka ishirini ya mazungumzo na mijadala serikali kutoka sehemu mbali mbali duniani hii leo zimeafikia makubaliano mapya ya kusimamia mali asili yenye umuhimu wa kiuchumi duniani .
Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa takriban watu milioni 7 bado hawana makao miezi mitatu baada ya mafuriko kuikumba Pakistan.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani kisa ambapo wafanyikazi wa mahakama inayoungwa mkono na UM iliyobuniwa kuwahukumu washukiwa wa mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri walishambuliwa na kukitaja kitendo hicho kama ambacho hakitakubalika.
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa hali inaendeea kuwa mbaya kaskazini mwa Kenya baada ya mamia ya wasomalia kuendelea kuingia nchini Kenya wakikimbia mapigano kati wanamgambo wa Al-Shabaab na kundi la Ahlu Sunna Wal Jamaa linaloegemea upande wa serikali ya mpito ya Somali kwenye mji wa mpaka wa Beled Hawo. George Njogopa na taarifa kamili
Karibu wakimbizi 47,000 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wamekuwa wakiishi nchini Zambia wamerejea nyumbani kwa hiari kwenye mpango ulioanzishwa miaka minne iliyopita na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa serikali ya Myanamar akiitaka iwachilie huru wafungwa wa kisiasa akisema kuwa bado kuna muda wa kuchukua hatua za kuleta uwiano wa kitaifa.
Wakati vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika nchi za Chad na Jamhuri ya Kati MINURCART vikiwa katika maandalizi ya kuondoka kwenye nchi hizo, Katibu Mkuu wa Umoja huo wa Mataifa ametia uzito haja ya kuziunga mkono nchi hizo ili ziweze kutatua matatizo yake zenyewe.
Chama cha msalaba mwekundu dunaini kimeanzisha mkakati wa dharura wenye shabaya ya kukusanya zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.4 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuruko Sudan ya Kusini, wanaofikia zaidi ya watu 50,000.
Mjumbe wa jopo huru la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza Frank La Rue ameelezea masikitiko yake kufutiwa kufungwa kwa waandishi wa habari 2 wa Panama ambao walitiwa hatiana baada ya kukutikana na kosa la kimazingira.