Habari Mpya

Matishio ya uharamia Usomali yamejizatiti bado licha ya kuwepo kwa manowari za kimataifa kwenye mwambao wa nchi

Asubuhi Baraza la Usalama liliitisha kikao cha hadhara kuzingatia ripoti ya karibuni ya KM juu ya hali ya uharamia na ujambazi wa baharini unaotendeka kwenye mwambao wa Usomali.

Ripoti ya UNFPA inasisitiza umuhimu wa wanawake katika kupiga vita mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) limeripoti Ijumatano kwamba, kwa kulingana na fafanuzi za taasisi yao, fungu kubwa la jamii ya kimataifa yenye kusumbuliwa, kwa uzito mkubwa kabisa na matatizo yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, huwa ni wanawake.

Mkuu wa UNIDO asema 'maendeleo ya viwanda ndio ufunguo wa kuiunganisha Afrika na uchumi wa dunia'

Kandeh K. Yumkella, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) amesihi kwamba bara la Afrika linahitajia kudhibiti vizingiti vya kiuchumi vinavyokwamisha maendeleo yao, kwa kukuza uzalishaji wa viwandani, hatua ambayo ikitekelezwa alisema huenda ikamegea Afrika sehemu kubwa zaidi ya natija za kiuchumi kutoka soko la kimataifa, na kunufaisha uchumi mzima wa ulimwengu wetu.

UM yahimiza Mataifa Wanachama yote kushirikiana kufyeka njaa duniani

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kwenye risala aliotoa mnamo siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula unaofanyika Roma, Utaliana, alisema raia wote wa kimataifa - na sio viongozi wa dunia pekee - wanawajibika kuhamasishwa wajitayarishe kuwapatia chakula watu bilioni moja ziada wenye kusumbuliwa na tatizo la njaa sugu ulimwenguni.

Natija za ubora wa hewa zitasailiwa kwenye Mkutano wa Sayansi ya Angahewa utakaofanyika Korea Kusini

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limearifu ya kuwa kikao cha kumi na tano cha Kamisheni juu ya Sayansi ya Angahewa, kitaanzisha mijadala maalumu mnamo siku ya Ijumatano, katika Korea Kusini.

ICTR imeamrisha kuachiwa kutoka vizuizini wafungwa wawili

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeamua kumwachia huru Hormisdas Nsengimana, aliyekuwa padri wa Rwanda, baada ya kuonekana hana hatia juu ya mashitaka ya kushiriki kwenye vitendo vya mauaji ya halaiki na makosa ya jinai dhidi ya utu na kuamrisha afunguliwe haraka kutoka Kituo cha UM cha Kuwekea Watu Kizuizini kiliopo Arusha, Tanzania.

Baraza la Usalama limelaani ongezeko la mashambulio ya LRA katika JKK

Ijumanne asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mashauriano kuhusu masuala ya eneo la Maziwa Makuu na tatizo la waasi wa Uganda wa kundi la LRA.

Mkuu wa Haki za Binadamu aisihi JKK kuwalinda mawakili, na watetezi wa haki za kiutu

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu ametoa taarifa yenye kuihimiza Serikali ya JKK kuhakikisha mawakili na watetezi wa haki za binadamu, ikijumlisha waandishi habari, huwa wanapatiwa ulinzi unaofaa utakaowaruhusu kutekeleza majukumu yao, bila ya kuingiliwa kati kikazi wala kubaguliwa, kutishiwa au kulipizwa kisasi kwa sababu ya shughuli zao.

OCHA inasema, hifadhi ya raia Kivu Kaskazini ndio jukumu muhimu kabisa kwa sasa

Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), Elizabeth Byrs, aliwaambia waandishi habari Geneva, leo hii, kwamba hali ya usalama katika Kivu, Majimbo ya Oriental na Equateur katika JKK, bado inaendelea kuwa mbaya zaidi.