Habari Mpya

Hapa na pale

Mjumbe wa KM anabashiria askari watoto wataachiwa na waasi katika JKK

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM Anayehusika na Hifadhi ya Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano ameripoti kuwepo maendeleo ya kisiasa ya kutia moyo hivi karibuni, katika JKK, ambayo alisema yamewakilisha fursa mpya itakayosaidia kuharakisha kuachiwa huru wale askari watoto waliokuwa wakidhibitiwa na makundi ya waasi wanaochukua silaha.

Mkuu wa UNHCR ashtumu sera za ubaguzi dhidi ya waombao hifadhi ya kisiasa

Ijumatano, Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliwaambia wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Geneva wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi Duniani, tangu kumalizika kwa Mkutano wa Awali wa Durban dhidi ya Ubaguzi miaka saba na nusu iliopita, waathirika wa mateso ulimwenguni bado wanaendelea kunyimwa hifadhi kwenye yale maeneo yenye uwezo wa kuupatia umma huo hali ya usalama.

Fujo za kikabila Sudan Kusini zaitia wasiwasi UNMIS

Shirika la UM Linalosimamia Ulinzi wa Amani Sudan Kusini (UNMIS) limeripoti kuingiwa wasiwasi mkuu kuhusu usalama wa eneo, baada ya kufufuka tena kwa mapigano ya kikabila kwenye Jimbo la Jonglei, ambapo inaripotiwa mnamo mwisho wa wiki iliopita darzeni za watu waliuawa, wenziwao kadha wa kadha walijeruhiwa na wengine kulazimika kukimbia makazi na kuelekea kwenye maeneo jirani.

Maambukizo ya Kipindupindu kusini mwa Afrika yaripotiwa kupungua na OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kuwepo mwelekeo wa kutia moyo kuhusu udhibiti wa maradhi ya kipindupindu kusini mwa Afrika. Ripoti imeeleza ya kuwa kasi ya maambukizo ya maradhi haya kieneo yanaendelea kuteremka.

Hapa na pale

Mataifa Wanachama yanayohudhuria Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi Duniani, unaofanyika wiki hii Geneva, Ijumanne yalipitisha, kwa ridhaa ya wote, ule waraka wa mkutano, hatua ambayo ilipongezwa kidhati na KM Ban Ki-moon.

ILO yaadhimisha miaka 90

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) linajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya kutimia miaka 90 tangu kubuniwa katika kipindi ambacho walimwengu hukabiliwa na mzozo mkuu wa fedha, ukichanganyika na ukosefu wa ajira.

UNEP inatayarisha mkutano wa kuzingatia upigaji marufuku madawa 12 ya kuuwa wadudu waharibifu

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) linatazamiwa kuandaa mkutano maalumu Geneva kusailia tatizo la afya, linalosababishwa na aina 12 za madawa yanayotumiwa kuuwa wadudu waharibifu wa mazo, madawa ya kemikali ambazo husemekana zinahatarisha afya ya wanadamu na kusababisha maradhi thakili ya saratani.

Idadi ya raia waliongolewa makazi na mashambulio ya waasi wa FDLR yakithiri JKK kuhudharisha UNHCR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumanne asubuhi aliwaeleza waandishi habari mjini Geneva kwamba mnamo wiki saba zilizopita idadi ya raia waliong\'olewa makazi ilikithiri pomoni, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya waasi wa kundi la FDLR, kwenye eneo la Lubero, Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).