Habari Mpya

Mtetezi wa mazeruzeru Tanzania ahimiza UM usaidie uimarishaji wa haki zao kimataifa

Kwenye wiki ya tarehe 20 mpaka 24 Aprili wajumbe kadha wa kadha kutoka Mataifa Wanachama wa UM walikusanyika mjini Geneva, Uswiss kuhudhuria Mkutano wa Maafikiano ya Durban kwa makusudio ya kutathminia, na pia kuharakisha, utekelezaji wa mapendekezo yaliopitishwa na kikao cha awali cha 2001, katika Durban dhidi ya ubaguzi.

Siku ya Kupiga Vita Malaria 2009

Ijumamosi, tarehe 25 Aprili itaadhimishwa rasmi kimataifa kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Malaria Duniani.

UNESCO yalaumu misaada ya ilimu ya msingi iliteremka 2007 katika nchi masikini

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeripoti mproromoko mkubwa wa misaada ya kuhudumia ilimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.

Raia wa JKK wanaendelea kuhajiri vijijini kukhofu adhabu za waasi wa Kihutu

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limesema lina wahka juu ya usalama wa umma ulionaswa kwenye mazingira ya uhasama katika eneo la mashariki la JKK, ambapo hali inasemekana inaendelea kuharibika. Hali hiyo imesababisha makumi elfu ya raia kuhajiri makaz, kutafuta usalama na hifadhi, katika siku za karibuni.

Mkutano juu ya Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi wahitimishwa Geneva

Mkutano wa Mapitio juu ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi, uliofanyika wiki hii mjini Geneva, Uswiss ulikamilisha shughuli zake leo Ijumaa. Kwenye mahojiano na waandishi habari wa kimataifa juu ya kikao hicho, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Bindamau, Navi Pillay alisema anaamini Mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa, licha ya kwamba mapatano yalikuwa magumu na yalichukua muda mrefu kukamilishwa.

Hapa na pale

WHO imethibitisha vifo vya malaria Zambia vimeteremka kwa asimilia 60 ziada

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti taifa la Zambia limefanikiwa kupunguza vifo vya malaria nchini kwa asilimia 66, kwa kutumia miradi maalumu ya dharura iliosaidia kudhibiti bora ugonjwa huu maututi.

Mkutano wa Brussels juu ya Usomali waahidi mamilioni kufufua amani

Kwenye Mkutano wa Kimataifa juu ya Usomali, uliofanyika kwenye mji wa Brussels, Ubelgiji Alkhamisi ya leo, wenye kuongozwa bia na Mwenyekiti wa UA, Jean Ping na KM wa UM Ban Ki-moon, uliwahamasisha wafadhili wa kimataifa kuahidi kuchangisha karibu dola milioni 250 kulisaidia taifa husika la Pembe ya Afrika kurudisha utulivu na amani ya eneo.

Abiria 35 wa mashua za magendo wameripotiwa na UNHCR kuzama Yemen

Taarifa ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imeeleza kwamba watu 35 waliripotiwa kuzama Ijumatano kwenye mwambao wa jimbo la Abyan, Yemen, liliopo kilomita 250 mashariki ya Aden, baada ya moja ya mashua mbili za wafanya magendo kupinduka.

Bei kuu ya chakula katika nchi masikini inaendelea kutesa mamilioni, kuhadharisha FAO

Kwenye ripoti iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) - yenye mada isemayo ‘Hali ya Chakula na Matarajiao ya Baadaye ya Mavuno\' - ilieleza kwamba bei ya juu ya chakula katika mataifa yanayoendelea inaendelea bado kusumbua na kuwatesa mamilioni ya umma masikini, raia ambao tangu mwanzo umeathirika na matatizo sugu ya njaa na utapiamlo, licha ya kuwa mavuno ya nafaka ulimwenguni, kwa ujumla, yameongezeka katika kipindi cha karibuni, na bei za chakula ziliteremka kimataifa, hali kadhalika.