Habari Mpya

Mataifa wanachama kuashiria mafanikio ya kuridhisha kuhusu Mkutano wa Durban

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu imearifu kuwa wawakilishi wa serikali wanachama wana imani ya kupatikana mafanikio ya kuridhisha katika kikao kijacho cha mapitio kuhusu masuala ya ukabila, ubaguzi wa rangi, matatizo ya chuki dhidi ya wageni na utovu wa kustahamiliana kitamaduni.

Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza tume ya uchunguzi juu ya ukiukaji sheria za kiutu Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limetangaza kumteua Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini kuongoza ile tume huru ya kuchunguza ukweli kuhusu ukiukaji wa sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu, na uvunjaji wa haki za kiutu, uliofanyika wakati mgogoro wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza ulipopamba mnamo miezi kichache iliopita.

Mabomu yaliotegwa yaendelea kuhatarisha watoto, kuonya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba mabomu yaliotegwa ardhini, pamoja na mabaki ya silaha zilizowachwa kwenye eneo la mapambano baada ya vita kumalizika, ni viripuzi vinavyoendelea babdo kuhatarisha maisha ya watoto katika kadha wa kadha ulimwenguni.

Hapa na pale

kwenye Mkutano Mkuu London na viongozi wa mataifa yenye uchumi mkuu, wanachama wa Kundi la G-20, uamuzi ambao waliahidi watachangisha furushi la dola trilioni 1.1, za kutumiwa kusuluhisha mzozo wa kiuchumi na fedha uliouvaa ulimwengu kwa hivi sasa. KM alitumai maafikiano ya G-20 yatayazipatia nchi masikini msaada maridhawa wa kufufua tena shughuli zao za maendeleo ya uchumi na jamii, kitaifa, kwenye maeneo yao.

IAEA imezikaribisha ahadi za Maraisi wa Urusi na Marekani kuzuia uenezaji wa silaha za kinyuklia duniani

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) ameingiwa matumaini makubwa na amezikaribisha ahadi za pamoja, zilizotolewa wiki hii na Raisi Dmitry Anatoleyevich Medvedev wa Shirikisho la Urusi pamoja na Raisi Barack Obama wa Marekani za kuchukua hatua hakika kutekeleza majukumu yao, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kinyuklia Duniani ili, hatimaye, kuuwezesha ulimwengu kuwa huru dhidi ya silaha za maangamizi ya halaiki za kinyuklia.

Wabuni sera za kimataifa wahimizwa na FAO kuwashirikisha wakulima kwenye mijadala ya Mkataba wa Kyoto

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limetoa taarifa yenye kuwahimiza wabuni sera za kimataifa kuhusu udhibiti wa athari za mabadiliko ya hali hewa duniani kujumuisha suala la kilimo pale wanapozingatia mkataba mpya utakaofuatia Mkataba wa 1997 wa Kyoto, baada ya kukamilisha muda wake.

Siku ya Kukumbushana Ugonjwa wa Autism yaadhimishwa na UM

UM leo unaadhimisha Siku ya Kukumbushana juu ya Ugonjwa wa Akili wa Watoto au kwa Kiingereza chake ugonjwa wa autism.

UM kuchangisha msaada wa kuihudumia Namibia kudhibiti athari za mafuriko

UM unajishughulisha hivi sasa kuchangisha dola milioni 2.7 zinazohitajika kuisaidia Jamhuri ya Namibia kudhibiti bora athari za mafuriko nchini, yaliosababishwa na mvua kali za karibuni ambazo zilin\'goa makazi watu 13,000 na pia kuharibu majumba na njia za kujipatia rizki kwa jumla ya watu 350,000.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amewasili London leo hii kuhudhuria mkutano mkuu wa mataifa wanachama wa kundi la G-20.

Wahamiaji walionusurika mwambao wa Libya wameripoti ajali yao ilisababishwa na hewa mbaya na woga wa abiria

Wale wahamiaji waliokolewa kutoka mashua ya wafanya magendo, iliopinduka mwanzo wa wiki nje ya mwambao wa Libya, wamewaambia wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ya kuwa boti yao ilizama kwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa mbaya, ikichanganyika na woga pamoja na khofu kubwa iliowavaa abiria, walipogundua kuvuja kwa mashua yao.