Habari Mpya

Kumbukumbu ya miaka 15 ya mauaji ya Rwanda kuadhimishwa na UM

Kadhalika, tarehe 07 Aprili 2009 inaadhimisha miaka 15 ya mauaji ya halaiki yaliotukia Rwanda katika 1994.

Siku ya Afya Bora Duniani kwa 2009

Tarehe ya Aprili 07, huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni Siku ya Afya Bora Duniani. Mwaka huu kumetolewa mwito maalumu na UM unaozihimiza serikali za kimataifa, kuwekeza zaidi kwenye mahospitali na kwenye vifaa na nyenzo nyengine za kutunza afya, vifaa ambavyo ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya umma wenye kuathirika na matatizo ya kiutu.

Hapa na pale

Hapa na pale

Wahudumia misaada ya kiutu Darfur watekwa nyara

Wafanyakazi wa kike wawili wenye kuhudumia misaada ya kihali Darfur Kusini, wanaowakilisha mashirika yasio ya kiserikali ya Ufaransa, Ijumapili usiku, walitekwa nyara kutoka makazi yao baada ya kushikiwa bunduki wao na walinzi, na majambazi wasiotambulika.

Mijadala leo katika Makao Makuu

Baraza la Udhamini leo linazingatia suala la mgogoro wa chakula duniani, na pia kujadilia sera za kutumiwa, kipamoja, na Mataifa Wanachama ili kuhakikisha haki ya mwanadamu kupata chakula hutekelezewa umma wa kimataifa kote ulimwenguni.

Siku ya afya duniani 2009 kuadhimishwa 07 Aprili

Ijumanne ya tarehe 7 Aprili huhishimiwa kimataifa kuwa ni Siku ya Afya Bora Duniani. Taadhima za 2009 zitalenga zaidi kwenye zile juhudi za kuimarisha usalama wa vifaa na nyenzo za kuhudumia afya ulimwenguni, na pia kwenye uwezo wa wahudumia afya katika mazingira ya tiba ya dharura.

KM asikitishwa na urushaji wa kombora angani na Korea Kaskazini

Ofisi ya Msemaji wa KM, kwenye ripoti iliotoa Ijumapili kwa waandishi habari, kuhusu kitendo cha kurusha kombora angani kilichofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini) hapo jana, taarifa hiyo ilibainisha masikitiko aliyokuwa nayo KM Ban Ki-moon juu ya kitendo cha Korea Kaskazini, ambacho alisema ilikwenda kinyume kabisa na nasaha za jumuiya ya kimataifa.

Hapa na pale

Uamuzi wa Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan (NEC) wa kufanyisha uchaguzi mkuu wa nchi katika mwezi Februari 2010, ni tangazo liliopokelewa kwa ridhaa kuu na KM, na amekitafsiri kitendo hicho kuwa ni kigezo muhimu katike utekelezaji wa Maafikiano ya Jumla ya Amani nchini.

Mawaziri wa Afya wakubaliana Beijing kuharakisha udhibiti bora wa TB sugu

Mkutano wa siku tatu, ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Umma wa Uchina pamoja na Taasisi za Bill na Melinda Gates, ulifanyika Beijing wiki hii, kwa makusudio ya kushauriana juu ya mradi mpya wa utendaji, utakaofaa kutekelezwa kipamoja ili kudhibiti bora maradhi ya kifua kikuu, hususan kwenye yale mataifa yanayosumbuliwa zaidi na ugonjwa huo.

Uamuzi wa Kenya kuwarejesha wahamiaji Usomali waitia wasiwasi UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuingiwa wasiwasi kuhusu mtindo wa karibuni wa Serikali ya Kenya wa kuwarejesha kwa nguvu Usomali, wale wahamiaji wenye kuomba hifadhi.