Habari Mpya

Idadi ya majongoo ya pwani imepungua ulimwenguni, yahadharisha FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti ya kuwa akiba ya majongoo wa pwani, au madondo, inaelekea kupungua ulimwenguni kwa kima cha kushtusha, hasa katika maeneo ya Afrika na kwenye Bahari ya Hindi ambapo uvuvi wa majongoo hawa imekiuka ada.

Wajumbe wa nchi 30 ziada wakutana Beijing kuzingatia tiba ya TB sugu

Mawaziri wa afya pamoja na wajumbe wa kutoka nchi 30 ziada wameanza kikao cha siku tatu mjini Beijing, Uchina kuzingatia namna ya kukabiliana na tatizo la kuemewa na maradhi sugu ya kifua kikuu yasiokubali dawa.

UNDP inayahimiza mataifa ya kundi la G-20 kuzingatia mahitaji ya umma wa nchi masikini kwenye majadiliano yao

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) wiki hii limetoa taarifa maalumu kwa viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la G-20, wanaokutana Alkhamisi mjini London, yenye kuwakumbusha ya kuwa mgogoro wa uchumi duniani huathiri zaidi maendeleo na maisha duni ya umma uliopo katika nchi masikini.