Habari Mpya

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amesema juhudi kubwa zaidi zinahitajika kote duniani kukomesha ghasia dhidi ya wanawake na wasichana, hasa kwa kuwahusisha zaidi wanaume na wavulana.

KM-uchaguzi wenye kasoro hatari kwa Afganistan

KM Ban ki-moon ameonya kwamba uchaguzi utakaokua na kasoro huko Afghanistan utaweza kurudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana, akitoa mwito kwa jumuia ya kimataifa kusaidia juhudi za kuimarisha uthabiti katika taifa hilo linalokumbwa na ghasia.

UM kuungana na kamati kubuni mpya kazi za mazingira

Mpango huo unatokana na jibu kwa pendekezo la waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, wakati wa mkutano wa viongozi wa Jopo la Uchumi huko Davos, Uswisi mwezi Januari, wa kundwa kwa kamati maalum ya kupunguza kiwango kikubwa cha utowaji gesi za carbon.

Msaada kamili unahitaji kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria

Ni lazima kugharimia kikamilifu Fuko la Global Fund kuweza kupambana dhidi Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria ikiwa nchi zinabidi kufikia lengo la kumpatia kila mtu Duniani uwezo wa kujikinga kutokana na HIV, matibabu, msaada na kuhuduma alisisitiza mkuu wa Shirika la UM la kupambana na Ukimwi UNAIDS.

UNHCR imeshtushwa na vifo vingi vya wahamiaji huko Mediterrenean

Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR limeelza kushtushwa kutokana na ripoti za kufariki na kupotea mamia ya wahamiaji nje ya pwani ya Libya walipokua wanajaribu kutafuta maisha mepya Ulaya.

Kuzorota ghasis huko Afrika ya kati kunasababisha maelfu kukimbia makazi yao

Kuongezeka kwa mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumesababisha maelfu ya wakazi kukimbia kutoka makazi yao kufuatana na idara ya huduma za dharura ya UM.

UM waonya kua vitongoji vya maskini kuongezeka mara tatu kutokana na mizozo ya kiuchumi

Akiufungua mkutano wa 22 wa shirika la Makazi la UM, UN Habitat, Makamu Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka alisema, kuna haja ya kusisitiza juu ya mipango na kugharimia ujenzi wa nyumba ambazo watu wa tabaka la chini wanaweza kumudu, ili kuweza kupata maendeleo ya kudumu katika miji.

FAO kupambana na ukame pembe ya Afrika

Kwa ushirikiano na Makundi yasiyo ya Kiserekali na Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, linafanya kazi kukabiliana na matatizo msingi yanyosababisha njaa huko Pembe ya Afrika.

Ban atowa mwito wa msaada zaidi kwa juhudi za kupambana na UKIMWI, TB NA Malaria

Katika wakati huu wa misukosuko ya kiuchumi, kugharimia vita dhidi ya UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria ni uwekezaji wa busara, alisema KM Ban Ki-moon hii leo alipowahimiza wafadhili kugharimia juhudi za UM kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo ya hatari.

UM yafungua vituo viwili vya uwokozi Bahari ya Hindi

Shirika la kimataifa la Safari za Baharini la UM IMO limefungua vituo viwili vipya vidogo vya kutafuta na kuokoa maisha ya watu baharini huko Tanzania na Ushelsheli, njee ya pwani ya Afrika ya Mashariki.