Habari Mpya

Shughuli za kulinda amani, kukaguliwa kwa kina wakati inakabiliwa na upungufu wa rasilmali

Kazi za kulinda amani za UM zinazokabiliwa na hali ambayo hayajapata kutokea na upungufu mkubwa wa rasilmali, zitakaguliwa kwa kina mnamo maka unaokuja kufuatana na mkuu wa Idara ya Kazi za Kulinda Amani DPKO.

Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM ahimiza mataifa kutanzua tofauti zao katika vita dhidi ya ubaguzi

Kamishina mkuu wa Haki za Binadamu wa UM Navi Pillay alisisitiza jana haja ya nchi wanachama kuweka kando tofauti zao na kufanya kazi pamoja kuushinda ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi nya wageni kabla ya mkutano wa pili wa Durban baadae mwaka huu.

KM alaani vikali mauwaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika

KM wa UM Ban Ki-moon alilaani vikali jana shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika AU huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia, lililosabibisha vifo vya walinda amani 11 wa Burundi.

Hapa na pale

Mjumbe maalum wa UM huko Somalia amesema alishutshwa na habari za shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko Mogadishu, siku ya jumapili lililosababisha vifo vya wanajeshi 11 wa Burundi.

Qatar yatoa $ milioni 40 kwa ajili ya misaada ya dharura

Serekali ya Qatar imetangaza hii leo kwamba imetoa msaada wa dola milioni 40 ili kusaidia mipango ya huduma za dharura ya UM kote duniani.

ILO yajadili athari za mzozo wa kiuchumi kwa wafanyakazi katika sekta ya fedha

Wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi na mashirika ya waajiri watakutana huko Geneva kesho, kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Kazi ILO kujadili athari za mzozo wa kiuchumi kwa zaidi ya wafanya kazi milioni 20 wa sekta za fedha kote duniani.

Majeshi ya AU na UM yaimarisha doria kuwalinda waliopoteza makazi yao

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur UNAMID kimeripoti leo kwamba kikosi chake cha polisi kitafanya doria ya kwanza wakati wa usiku kutokea kituo kipya cha polisi katika jamii CPC kilichojengwa kati kati ya makambi mawili makubwa ya watu walopoteza makazi yao IDP\'s karibu na mji wa El Fasher mji mkuu wa Darfur ya Kaskazini.

Mjumbe maalum wa UM awataka wanamgambo wa Kihutu kuondoka Kongo

Mjumbe maalum wa UM huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewahimiza tena wapiganaji wa kihutu kutoka Rwanda katika jimbo lenye misukosuko la Kivu ya Kaskazini, kuweka chini silaha zao na kurudi nyumbani.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu itatangaza uwamuzi wa kukamatwa au la kwa Rais wa Sudan hivi karibuni

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitangaza Jumatatu kwamba itatoa uwamuzi wake kuhusu kutowa kibali cha kukamatwa Rais Omar al Bashir wa Sudan hapo march 4, 2009.

UM yarudia mwito wa kuachiwa afisa aliyetekwa nyara Pakistan

UM umerudia tena mwito wake wa kutaka kuachiliwa kwa afisa mmoja wa UM aliyetekwa nyara huko kusini magharibi ya Pakistan.