Habari Mpya

Baraza la Usalama lakutana tena kusailia mgogoro wa Ghaza

Baraza la Usalama limekutana Ijumatano magharibi, kwenye kikao cha dharura, kuzingatia mswada wa azimio liliodhaminiwa na Libya, kwa niaba ya Mataifa Wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za KiArabu, kuhusu uwezekano wa kusimamisha mapigano yaliozuka katika eneo la WaFalastina liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza. Kwenye risala mbele ya kikao hicho, KM Ban Ki-moon alikumbusha ya kuwa mtiririko wa mgogoro uliofumka Ghaza siku ya leo umeingia siku ya tano. Alisema raia wa KiFalastina, wanaojumuisha mfumo wa jamii hakika ya Tarafa ya Ghaza, pamoja na mpango wa amani kwa siku za

KM na wadau wa kidiplomasiya wasisitiza mapigano yasimamishwe haraka Ghaza na Israel kusini

Ijumanne KM Ban Ki-moon alifanya mazungumzo, kwa kutumia njia ya mawasiliano ya televisheni, na wawakilishi wa kundi la wapatanishi wa pande nne kuhusu amani Mashariki ya Kati, ikijumlisha UM yenyewe, Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani.

Mkuu wa UNRWA asema hali, kijumla, ni 'mbaya sana' kwa sasa Ghaza

Kwenye mahojiano na Idara ya Habari ya UM Ijumanne, Karen AbuZayd, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) alieleza ya kuwa hali ya vurugu katika Tarafa ya Ghaza hivi sasa, ni mbaya sana kushinda mifumko ya uhasama wa miaka iliopita, kwenye eneo hilo:~

Kiini cha matatizo ya Usomali ni ukosefu wa uongozi imara, asisitiza Mjumbe wa KM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah amewatumia umma wa Kisomali, uliotawanyika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu, barua yenye kueleza kwamba chimbuko la matatizo ya taifa lao linatokana na ukosefu wa uongozi imara wa kisiasa, uongozi uliojihusisha kidhati na masuala ya kijamii, na wenye kujali majukumu ya kitaifa.

Mabadiliko ya uwanachama kwenye BU kwa 2009

Leo ni siku ya mwisho ya uwanachama wa katika Baraza la Usalama kwa mataifa ya Ubelgiji, Indonesia, Utaliana, Panama na Afrika Kusini.

Hapa na Pale

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kwamba Ban Ki-moon anaendelea kushauriana, kwa kutumia njia ya simu, na maofisa wa UM wa vyeo vya juu waliokuwepo kwenye eneo la uhasama Mashariki ya Kati. Katika saa 24 zilizopita KM aliwasiliana na mawaziri wa nchi za kigeni wa Israel na Marekani, na KM anatazamiwa kuongeza juhudi zake katika siku zijazo katika kuhakikisha mwito wa kusimamisha mapigano katika eneo liliokaliwa la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza utahishimiwa.

Vikosi vya AMISOM Usomali vyapongezwa na KM kwa ujasiri wao

KM Ban Ki-moon amerudia tena mwito alioutoa hapo kabla, unaoyahimiza Mataifa Wanachama kuharakisha kuchangisha misaada ya fedha, pamoja na ile misaada inayohitajika kushughulikia usafirishaji wa watu na vitu, au lojistiki, ili kuhudumia bora operesheni za vikosi vya Umoja wa Afrika katika Usomali, yaani vikosi vya AMISOM.

Taathira za makombora Ghaza, dhidi ya watoto, zaitia wasiwasi UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa taarifa inayobainisha wahka mkuu kuhusu kihoro kilichowapata watoto kutokana na athari ya vurugu liliolivaa sasa hivi eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.

Upungufu wa matibabu Ghaza unaashiria ongezeko la vifo kwa majeruhi, WHO imeonya

Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye taarifa iliochapishwa Ijumanne ya leo, limeonya ya kuwa mamia ya majeruhi katika hospitali za Tarafa ya Ghaza wanakabiliwa na hatari ya ongezeko kubwa la vifo vinavyozuilika, kwa sababu ya ukosefu wa madawa.

Ripoti ya UNODC yathibitisha mauaji yamekithiri Kusini ya Afrika na Amerika za Kati na Kusini

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imechapisha ripoti mpya kuhusu viwango vya mauaji ulimwenguni.