Habari Mpya

Kumbukumbu za miaka 10 ya uongozi wa KM mstaafu Kofi Annan katika UM (Sehemu ya Pili)

Sehemu ya pili ya makala hii inaendelea na mahojiano aliyokuwa nayo KM mstaafu Kofi Annan na wanahabari wa kimataifa kwenye kikao cha mwisho kabla ya kukhitimisha kazi na Umoja wa Mataifa (UM).

Kumbukumbu za miaka 10 ya uongozi wa KM mstaafu Kofi Annan katika UM (Sehemu ya Kwanza)

KM mstaafu Kofi Annan, siku chache kabla ya kumaliza uongozi wake wa miaka 10 katika Umoja wa Mataifa, aliitisha kikao cha mwisho cha mahojiano na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu mjini New York. Alizungumzia masuala mbalimbali na kuchambua taratibu zinazohitajika kutekelezwa ili kuboresha uhusiano wa kimataifa miongoni mwa Mataifa Wanachama.

Ziara ya Katibu Mkuu katika Ikulu ya Marekani

Ijumanne KM Ban Ki-Moon alizuru Ikulu ya Marekani mjini Washington DC na kufanya mkutano rasmi, wa awali, na Raisi wa Marekani George Bush. Ziara hiyo ilihusika na hishima za kidiplomasia kwa Serekali Mwenyeji wa UM, yaani Serekali ya Marekani, ziara ambayo KM mpya anawajibika kuikamilisha.~

Huduma za Umoja wa Mataifa katika kufufua utulivu na amani Usomali

Mapema wiki hii UM ulipeleka tume maalumu ya ukaguzi, kwenye mji wa Mogadishu, Usomali kwa mara ya kwanza tangu Serekali ya Mpito kuchukua madaraka. Dhamira ya ujumbe huo ni kutathminia mahitaji ya misaada ya kiutu kwa raia wa Usomali.

Baraza la Usalama lapendekeza kuchukuliwe hatua za dharura katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Januari, Balozi Vitaly Churkin wa Shirikisho la Urusi aliwaambia waandishi habari waliopo Makao Makuu ya UM kwamba wajumbe wa mataifa 15 katika Baraza hilo walikubaliana kupendekeza kwa KM Ban Ki-moon atayarishe haraka tume ya utangulizi itakayozuru Chad na pia Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mashauriano na serekali za mataifa haya mawili. Baadaye KM alitakiwa atayarishe ripoti ya mapema itakaousaidia UM kuandaa operesheni za ulinzi wa amani katika eneo lao.

Waathiriwa wa ukame 500,000 Uganda kuhudumiwa chakula na WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha operesheni za kuwahudumia chakula watu 500,000 muhitaji wa eneo la Karamoja, katika Uganda ya kaskazini-mashariki.

ICTR imeamua kuendeleza kifungo cha maisha kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) iliopo Arusha, Tanzania imeamua kuendeleza kifungo cha maisha dhidi ya Emmanuel Ndindabahizi, aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Rwanda.

Kumbukumbu za mkutano wa awali wa KM mpya na vyombo vya habari

KM Ban Ki-moon alifanyisha mkutano rasmi wa kwanza na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa waliopo Makao Makuu ya UM mjini New York mnamo Alkhamisi ya tarehe 11 Januari 2007. KM Ban aliwafafanulia ratiba ya masuala aliyokabiliana nayo siku 10 baada ya kuchukua madaraka ya kuongoza taasisi hii muhimu ya kimataifa.

UM waashiria mwelekeo wa uchumi wa dunia kwa 2007

Katika kila mwanzo wa mwaka, UM huwasilisha ripoti maalumu kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uchumi duniani, ripoti ambayo huandaliwa na idara mbalimbali za UM, ikijumuisha Idara Inayohusika na Masuala ya Kiuchumi na Jamii (DESA), Shirika la UM kuhusu Maendeleo ya Uchumi na Biashara (UNCTAD) pamoja na kamisheni tano za kikanda zinazoshughulikia huduma za uchumi, yaani Kamisheni ya ECA, kwa Afrika, ECE, kwa Mataifa ya Ulaya, ECLAC, kwa Amerika ya Latina na Maeneo ya Karibiani, ESCAP, kwa mataifa ya Asia na Pasifiki na vile vile Kamisheni ya ESCWA, inayohusika na maendeleo ya Asia ya Magharibi. ~~

Mtumishi wa WFP kuuawa baada ya mashambulio ya kuvizia Sudan ya kusini

Emmanuel Chaku Joseph, mwenye umri wa miaka 28, raia wa Sudan aliyeajiriwa udereva na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) aliuawa kikatili mnamo kati ya wiki baada ya kuzingiwa na kushambuliwa kwenye barabara kati ya Juba, mji mkuu wa Sudan kusini na mji wa Torit.