Habari Mpya

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewaslisha wiki hii mjini Roma, Utaliana ripoti yenye mada isemayo "Hali ya Misitu Duniani 2007". Ripoti ilisema maeneo kadha duniani yamefanikiwa kudhibiti uharibifu wa misitu ulioendelezwa karne kwa karne. Kwa mujibu wa ripoti misitu kadha imefanikiwa kufufuliwa na kupanuliwa kwenye kanda mbalimbali za kimataifa kwa sababu ya usimamizi mzuri, na wa hadhari, ikichanganyika na sera za kisasa zilizotumiwa na mataifa husika katika kuhifadhi mazingira kwa ujumla. Ripioti ilisema mataifa 100 ziada hivi sasa yameandaa mipango ya kizalendo kuhifadhi misitu.

Sikukuu ya Wanawake wa Kimataifa

Tarehe 08 Machi kila mwaka huadhimishwa na walimwengu kuwa ni Sikukuu ya Wanawake wa Kimataifa. Hapa kwenye Makao Makuu ya UM, mjini New York, kulifanyika taadhima mbalimbali za kuiheshimu siku hiyo, zikijumuisha mikutano, warsha za wataalamu na tafrija aina kwa aina.

Mjumbe wa Kenya achambua kikao cha mwaka cha Kamisheni ya CSW

Kamisheni ya Haki za Wanawake, au Kamisheni ya CSW, ilikutana kwa muda wa wiki mbili kwenye Makao Makuu, mjini New York, katika kikao cha mwaka kuanzia tarehe 26 Februari hadi tarehe 09 Machi (2007). Kikao cha 2007 ni cha 51.

WFP inabashiria tatizo la njaa kusini ya Afrika

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuingiwa na wasiwasi unaoashiria kufumka, kwa mara nyengine tena katika maeneo ya kusini ya Afrika, janga la njaa kwa sababu ya kujiri karibuni kwa hali ya hewa ya kigeugeu. Hali hii imezusha ukame na mafuriko ambayo yaliharibu mavuno na kuathiri mamilioni ya watu watakaotegemea kusaidiwa chakula na jamii ya kimataifa kwa mwaka mzima.

Makundi yote DRC yaharamisha haki za kibinadamu, imeripoti UM

Ofisi ya UM juu ya Haki za Kibinadamu ya Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) WIKI HII imetoa ripoti maalumu kuhusu namna haki za kimsingi zinavyotekelezewa raia kwa ujumla.

Uvamizi wa polisi wa Mahakama Kuu Uganda umelaumiwa na UM

Ofisi ya UM juu ya Haki za Kibinadamu nchini Uganda imetoa mwito maalumu kwa Serekali kuheshimu uhuru wa mahakama. Mwito huu ulitolewa baada ya askari polisi wenye silaha walipovamia Mahakama Kuu mjini Kamapala, hivi majuzi, na kuwatia mbaroni, kwa mara nyengine tena, wale raia wafuasi wa Kundi la People\'s Redemption Army (PRA), baada ya raia hao kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Kampala. Ofisi ya UM imesisitiza ya kuwa "mahakama ilio huru kuendeleza shughuli zake ndio ufunguo hakika wa kuimarisha utaratibu wa kufuata sheria katika jamii huru ya kidemokrasia."

WFP imewaomba maharamia kuachia huru mabaharia wa meli yake

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limewaomba wale maharamia walioteka nyara karibuni ile meli iliokodiwa kupeleka chakula Usomali, wawaachie huru mabaharia na chombo chao ili waweze kuendelea kuhudumia kihali ule umma muhitaji wa eneo hilo la Pembe ya Afrika. Meli ya WFP iliyotekwa nyara imeripotiwa kutia nanga katika eneo liliopo karibu na Puntland, Usomali.~

Mjumbe wa UM kwa Darfur asisitiza mapigano lazima yakomeshwe halan kabla amani kuwasili

Balozi Jan Eliasson wa Usweden Mjumbe Maalumu wa KM kwa Darfur, ambaye mwezi uliopita alizuru Sudan pamoja na Mpatanishi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, AU, Salim Ahmed Salim kutafuta suluhu ya kuridhisha mapema wiki hii aliripoti juu ya ziara yao kwenye kikao cha faragha cha Baraza la Usalama.

KM kuhimiza suluhu ya amani kwa Darfur

KM Ban Ki-moon amemtumia Raisi Omar Hassan Al Bashir wa Sudan, kwa mara nyengine tena barua yenye kuelezea, kwa ukamilifu, utaratibu na hatua za kuchukuliwa zitakazorahisisha ile rai ya kupeleka vikosi vya mseto vya ulinzi wa amani vya UM na AU katika Darfur, majeshi ambayo idadi yao inakadiriwa kufikia askari 24,000.

Baraza la Usalama linasailia suala la Maziwa Makuu

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Masuala ya Maziwa Makuu, Ibrahima Fall aliripoti mbele ya Baraza la Usalama mwisho wa wiki kuhusu maendeleo ya kurudisha utulivu na amani kwenye eneo hili muhimu la Afrika.