Habari Mpya

Mahojiano na Naibu Katibu Mkuu wa UMoja wa Mataifa, Dktr Asha-Rose Migiro

Hivi majuzi, wasikilizaji, tulikuwa na mazungumzo maalumu kwenye studio zetu za Redio ya UM na Naibu KM wa UM Asha-Rose Migiro.

Mataifa Wanachama yasailia tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Wawakilishi kutoka nchi mataifa 150 ziada, walijumuika kwenye Makao Makuu ya UM kujadilia tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa duniani, na namna ya kukabiliana na suala hili kwa taratibu zitakazoletea natija, badala ya madhara, kwa umma wa kimataifa. Kikao hiki muhimu kiliandaliwa na KM Ban Ki-moon.

Baraza la Usalama latathminia amani na usalama wa Afrika

Viongozi wa Kitaifa, wakijumuika na wakuu wa Serekali pamoja na mawaziri wa vyeo vya juu kutoka nchi 15 zilizo wanachama wa Baraza la Usalama, pamoja na KM wa UM Ban Ki-moon na Mwenyekiti Alpha Oumar Konare wa Umoja wa Afrika (AU) walikusanyika mapema wiki hii kwenye Baraza la Usalama kujadilia njia bora za kurudisha utulivu wa amani na usalama katika Afrika, eneo ambalo linadaiwa kuwa na vurugu na migogoro ya kila aina.

Baraza Kuu laanza rasmi mjadala wa wawakilishi wote

Ijumanne, tarehe 25 Septemba (2007) wajumbe wa kimataifa walianza rasmi mahojiano ya mwaka kwenye kikao cha wawakilishi wote kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la UM. Kikao cha mwaka huu ni cha 62, na wajumbe kutoka Mataifa Wanachama kadha wa kadha waliwasilisha sera zao za kitaifa kuhusu hatua wanazochukua kukabiliana na matatizo yanayosumbua walimwengu.~~Raisi mpya wa Baraza Kuu, Srgjan Kerim, kutoka Jamhuri ya Yugoslavia ya Zamani ya Macedonia pamoja na KM wa UM, Ban Ki-moon walijumuika na viongozi mbalimbali wa Nchi Wanachama kuzingatia taratibu za kuchukuliwa kipamoja kustawisha uhusiano mwema wa kimataifa.

Wataalamu wa UM walaumu haki za binadamu zinakiukwa Darfur

Wataalamu saba wa tume ya UM wenye dhamana ya kufuatilia namna haki za binadamu zinavyotekelezwa katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur wamewakilisha wiki hii ripoti ya muda mjini Geneva mbele ya Halmashauri ya Haki za Binadamu.

WFP kununua mahindi Lesotho kusaidia Liberia

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kununua mahindi kutoka wakulima wadogo wadogo wa Lesotho, mahindi ambayo yatatumiwa kuwapatia chakula na lishe bora kwa maelfu ya watoto wa skuli za praimari katika Liberia.

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali kuzuru Mogadishu

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Usomali, Ahmed Ould Abdallah karibuni alifanya ziara rasmi Mogadishu na kuwa na mazungumzo na viongozi wa Serekali ya Mpito, wakiwemo Raisi na Waziri Mkuu. Abdallah kwenye majadiliano yake aliyahimiza makundi yote husika na mgogoro wa Usomali kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya ule mwafaka wa Mkutano wa Upatanaishi wa Taifa.

Vikosi vya amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baraza la Usalama limepitisha azimio muhimu lilioruhusu vikosi vya ulinzi wa amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa katika Chad mashariki na sehemu za mashariki-kaskazini ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Vikosi hivi vinatazamiwa kuwapatia raia wa maeneo hayo hifadhi, na vile vile kuwapatia wahamiaji na umma uliong’olewa makwao ulinzi bora dhidi ya mashambulio ya kihorera.

Watoto milioni 2 wamefanikiwa kuchanjwa shurua na polio Uganda

UM umeripoti kwamba Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) pamoja na mashirika wenzi kadha wamefanikiwa kuwachanja watoto milioni 2 nchini Uganda dhidi ya maambukizo ya shurua na polio.

Tume ya Ushirikiano wa Tamaduni za Kimataifa yakutana Makao Makuu

Kundi la Marafiki wa Tume ya Ushirikiano wa Kitamaduni, iliyobuniwa shirika na serekali za Uturuki na Uspeni, ilikutana kwenye kikao maalumu wiki hii kwenye Makao Makuu ya UM kilichohudhuriwa na mawaziri.