Habari Mpya

Operesheni za amani za UNMIS na MINURSO zimeongezewa muda

Baraza la Usalama limepitisha maazimio mawili ya kuongeza muda wa operesheni za ulinzi wa amani za UM katika Sudan Kusini (UNMIS) na katika Sahara ya Magharibi(MINURSO) kwa miezi sita ziada, hadi mwisho wa Oktoba 2007. Muda wa operesheni hizo ulimalzika tarehe 30 Aprili.

Hapa na pale

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeanzisha mradi mpya utakaotumiwa kuwakinga wagonjwa dhidi ya hatari ya makosa wakati wanapopimwa afya, hasa ilivyokuwa mgonjwa mmoja katika kila wagonjwa 10 kwenye nchi zinazoendelea hudhurika kiafya, kwa sababu ya utambuzi wa maradhi usio sahihi.~