Habari Mpya

Tume ya Kudumu ya Haki za Wenyeji as Asili inakutana Makao Makuu

Wawakilishi zaidi ya 1,000 walio wenyeji wa asili, kutoka sehemu kanda mbalimbali za dunia, walikusanyika kuanzia mwanzo wa juma, katika Makao Makuu ya UM mjini New York, kuhudhuria kikao cha wiki mbili cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili.

Muda wa operesheni za UM katika DRC umeongezwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (DRC), yaani MONUC, hadi mwisho wa mwaka. Huduma za ulinzi wa amani za MONUC zinatarajiwa kuimarisha vizuri zaidi hali ya utulivu katika eneo hili la Afrika ya Kati.

Maofisa wa UM washtumu mauaji ya wanajeshi 4 wa Uganda katika Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Francois Lonseny Fall ameshtumu vikali mauaji ya wanajeshi 4 wa Uganda wa vikosi vya ulinzi wa amani vya AU, yaliotokea hivi majuzi mjini Mogadishu, Usomali.

WFP itaongeza huduma za chakula Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha operesheni ziada kuhudumia chakula watu 122,500 nchini Usomali, wingi wao wakiwa watoto wadogo na wanawake, ambao waliathirika kihali kutokana na mapigano yaliofumka karibuni kwenye maeneo yao.

Mradi wa kudhibiti homa ya manjano kuanzishwa na WHO Afrika Magharibi

Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo linakutana sasa hivi Geneva, Uswiss limepitisha mradi wa kuanzisha kampeni ya kudhibiti homa ya manjano katika mataifa 12 yaliopo Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa WHO maradhi ya homa ya manjano yaligunduliwa kuibuka katika baadhi ya sehemu za Afrika Magharibi na kunahitajika juhudi za dharura kuyadhibiti yasije yakafumka kwa kasi na kulitapakaza janga hilo kwa umma uliobanwa na matatizo kadha mengineyo ya kiuchumi na jamii.

KM Ban anayahimiza makundi ya Cote d'Ivoire kutekeleza kikamilifu maafikiano ya amani

Ripoti ya KM kuhusu Cote d’Ivoire iliotolewa karibuni imeelezea juhudi na hatua zilizochukuliwa na wenye madaraka nchini katika kuvitekeleza vifungu vya Mapatano ya Ouagadougou ya kurudisha utulivu na amani ya taifa lao.

Msaada zaidi unahitajika Bukini baada ya maafa ya tufani

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA)imeripoti kuwa imewajibika kuomba msaada zaidi wa dola milioni 20 kwa Bukini, kukidhia mahitaji ya kihali ya umma ulioathirika na maafa yaliosababishwa na kimbunga kilichopiga huko mnamo miezi miwili iliopita.

Hapa na pale

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alihimiza viongozi na wajumbe waliohudhuria kikao cha mwaka cha sita cha bodi linaloandaa sera na miradi ya afya ya kimataifa, kinachokutana hivi sasa Geneva, Uswiss kwamba kunatakikana hima kuu ya jumla kutoka kwao wote, kujenga kile alichokiita “urithi wa afya”, kadhia ambayo alitumai ikikamilishwa itasaidia kuaboresha siha za wanawake na afya ya umma wa Afrika, kwa ujumla; kwa sababu, Dktr Chan anaamini kidhati kuwa wanawake ni fungu muhimu la umma wa kimataifa, linaloongoza kwenye harakati kadha wa kadha za maendeleo ulimwenguni.

-- Juhudi za kuboresha biashara ya maji ya madafu kwa kutumia teknolojia ya kisasa -- Pendekezo la kudhibiti biashara ya silaha ndogo ndogo ulimwenguni

Watu wenye kuishi kwenye maeneo ya joto, na karibu na minazi – au wale wenye uwezo wa kununua madafu kutoka wachuuzi wa kwenye miji - hutambua vyema kwamba maji ya madafu ni kinywaji kinachoburudisha sana, chenye natija kwa afya na pia kina ladha tamu kabisa.

Athari za nishati ya vitu hai kuzingatiwa na UM

Nishati ya kisasa, ya vitu hai (bioenergy), ina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya umeme na kuboresha ,aisha ya watu bilioni 1.6 kote duniani, na vile vile ina uwezo wa kuwapatia umeme watu bilioni 2.4 ziada ambao kawaida hutegemea nishati za kijadi zinazotokana na mabaki ya wanyama na mimea.