Mimi na wewe sote tunawajibika kulinda bayoanuai: Mrema
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba bayoanuai ya dunia inaendelea kupotea na endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa sasa basi mustakbali wa viumbe vya dunia wakiwemo binadamu, mazingira na sayari yenyewe kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo utakuwa njiapanda.